27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Samia alia na alama ‘V’

IMG_0273 (1280x853)NA SARAH MOSSI, KOROGWE

 

MGOMBEA mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan amesema alama ya ‘V’ haijawahi kushika dola duniani kote.

Samia, alisema hayo jana  alipokuwa akizungumza na wananchi katika eneo la Mombo akiwa njiani kuelekea wilayani Lushoto.

“Sasa hivi vurugu tupu, utawala wa nchi si wa kujaribu, wapeni wenye uthabiti, waliosimama imara na  uwezo ndugu zangu, sumu haionjwi,”alisema Samia.

Mapema akiwahutubia wananchi wa Korogwe mjini katika viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi, Samia alisema Serikali inafanya mapitio ya uwiano wa mishahara kwa watumishi wa umma ili viandane na halisi ya maisha.

Alisema Serikali inatambua malalamiko ya watumishi wake, wakiwamo walimu madaktari na wauguzi.

Alisema kama wakichaguliwa watahakikisha wanshughulikia matatizo hayo haraka iwezekanavyo bila kinyongo.

Akizungumzia tatizo la maji wilayani Korogwe, alisema mradi mkubwa wa maji wilayani humo mapendekezo yake yamefikishwa kwa rais.

 

“Sifurahishwi kuona wanawake wanatembea umbali mrefu kutafuta maji nawaahidi awamu ya tano itauchukua mradi huo na kuukamilisha,” alisema Samia

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles