24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Samia aeleza malengo ya serikali kusambaza maji

Mwandishi wetu. Kibaha

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu, amesema Serikali ya awamu ya tano imeendelea kutekeleza ahadi ya kusambaza maji mjini na vijijini.

Alisema  mpaka ifikapo mwaka 2020 inategemea maji yatakuwa yamefika vijijini kwa asilimia 85 na mjini asilimia 90.

Samia  aliyasema hayo wakati akikagua ujenzi wa tanki la mradi wa maji Bagamoyo lenye uwezo wa kubeba lita milioni sita ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku sita mkoani Pwani.

Aliipongeza  Dawasa kwa kazi hiyo na amewataka wananchi kupitia kamati mbalimbali za maji kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji, miundombinu  na mazingira yake.

“Wote tujitahidi kutunza vyanzo vya maji,” alisema Makamu wa Rais.

Tanki hilo la Bagamoyo linatarajiwa kuhudumia wakazi wote wa mji wa Bagamoyo na vitongoji vyote vinavyozunguka mji huo.

Makamu wa Rais pia alitembelea mradi wa uzalishaji na usambazaji vifaranga wa Kampuni ya AKM Glitters na kuzungumza na wananchi waliojitokeza kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Majengo.

Katika ziara hiyo, Makamu wa Rais aliongozana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na viongozi wengine.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles