27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Samatta akosa ulaji Ulaya

Samata Bwana
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta

Na Abducado Emmanuel, Dar es Salaam

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, anayechezea timu ya mabingwa wa Ligi Kuu DR Congo, TP Mazembe, amesema ushiriki wa timu yake kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika umemnyima ulaji wa kwenda kukipiga Ulaya.

Samatta alikuwa miongoni mwa nyota wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ waliotoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Msumbiji, kwenye mechi ya raundi ya pili ya kuwania nafasi ya kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco.

Akizungumza na MTANZANIA, Samatta alisema kuna timu barani Ulaya ilikuwa tayari kumsajili baada ya kumalizika kwa Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Brazil, lakini akabanwa na ushiriki wa Mazembe kwenye michuano ya Afrika na kushindwa kujiunga nayo.

“Nilipata timu Ulaya ya kunisajili baada ya Kombe la Dunia, sema bosi Moisse Katumbi aliniambia bado Mazembe ipo kwenye michuano ya Afrika na mchango wangu unahitajika, hivyo akaniambia nisubirie yatakapomalizika ndo majaliwa na kujiunga na hiyo timu yatakapojulikana,” alisema Samatta.

Wiki iliyopita Samatta aliliambia gazeti hili kuwa kuna timu nyingi za Ligi Kuu ya Ufaransa na Ubelgiji zinamwania, huku akidai tayari ameshakubaliana na bosi Katumbi kuhusu yeye kutimkia Ulaya na amemkubalia.

Akizungumzia kwa ufupi mechi dhidi ya Msumbiji, Samatta alisema: “Mechi ilikuwa ngumu, tumepigana na tumeambulia sare hiyo, tutajipanga mechi ya marudiano na naamini kama wao waliweza kufanya vizuri hapa, hata sisi hatutashindwa kuwatoa kwao,” alisema Samatta.

Mazembe ipo kwenye Kundi A katika Ligi ya Mabingwa Afrika, inaongoza kundi hilo lenye timu za Al Hilal ya Sudan, AS Vita ya DR Congo na Zamalek ya Misri, ambapo itacheza na Zamalek Jumapili hii nchini Misri.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles