28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Samatta aingia 2019 kwa kishindo

MWANDISHI WETU –UBELGIJI

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, ameiongoza timu yake ya KRC Genk kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Sint-Truiden, katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji uliochezwa Uwanja wa Sint-Truiden, St. Trond.


Kwa ushindi huo, Genk ambayo huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza kwa mwaka 2019, ilifikisha pointi 51, baada ya kucheza mechi 22 na kuendelea kuongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 10 na Club Brugge iliyoko nafasi ya pili. 

Katika mchezo huo, Samatta, alifunga bao moja, huku akitengeneza jingine.

Samatta alifunga bao lake dakika ya 29, akimalizia pasi ya mshambuliaji, Dieumerci N’Dongala, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Bao hilo lilikuwa la kusawazisha baada ya Jordanaa Botaka ambaye pia nia raia wa DRC kuifungia Sint-Truiden bao la kuongoza dakika ya pili ya mchezo huo.

Mfaransa, Yohan Boli, aliifungia Truiden bao la pili dakika ya 70 kabla ya Samatta kumpa pande safi mshambuliaji Mbelgiji, Leandro Trossard, ambaye aliifungia bao la kusawazisha Genk dakika ya 75.

Genk ilipata nguvu zaidi baada ya kusawazisha na kufanikiwa kuandika bao la ushindi dakika ya 80 kupitia kwa Mkongomani, N’Dongala, aliyemalizia pasi ya Trossard.

 Samatta alipumzishwa dakika ya 90 na nafasi yake kuchukuliwa na  Zinho Gano.

Samatta mwenye umri wa miaka 26, amefikisha mabao 55 katika mechi 138 za mashindano yote alizoichezea KRC Genk tangu alipojiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya DRC.

Kwenye Ligi ya Ubelgiji ametupia mabao 40 katika mechi 106, wakati Europa League amefunga mabao 14, katika mechi 22 na katika Kombe la Ubelgiji amefunga mabao mawili katika mechi tisa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles