23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

RWANDA KUONGOZWA NA SERIKALI MBILI

PARIS, UFARANSA


HATUA ya kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, Thomas Nahimana kutangaza kuunda Serikali mbadala, kutalifanya taifa hilo kuwa na Serikali mbili tofauti.

Hata hivyo, kasisi huyo wa zamani wa Dayosisi ya Cyangugu, ameunda Serikali hiyo ikitarajia kufanya kazi ikiwa uhamishoni.

Awali Novemba mwaka jana, Nahimana anayeishi uhamishoni katika Jiji la Le Havre nchini hapa, tangu mwaka 2005, alitangaza dhamira yake ya kuwania urais kwa tiketi ya Chama cha Ishema.

Lakini dhamira yake hiyo inaonekana kugonga mwamba baada ya kukatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha kuwa mgombea wa kiti cha urais kwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Agosti.

Alizuiwa mara mbili mapema mwaka huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya akiwa njiani kuunganisha ndege kuelekea Rwanda.

Katika mazungumzo na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), mwanasiasa huyo alisema lengo la Serikali yake mpya ni kuiondoa madarakani Serikali ya Rais Paul Kagame.

Anamlaumu Rais Kagame kwa uvunjaji wa sheria na haki za binadamu pamoja na kukandamiza raia wake.

Baadhi ya aliowataja katika baraza lake la mawaziri, ni wafungwa wanaotumikia vifungo vya jela nchini Rwanda kwa makosa kama  kukanusha kufanyika kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Nahimana ambaye ni Mhutu, amekuwa akilaumiwa kwa kuandika na kusambaza taarifa kadhaa za kikabila na kumkosoa Rais Kagame. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles