27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ruka-Kipro yajikita kuwapa uzoefu wahitimu masomo ya sanaa

Vijana wakiwa kwenye programu ya Ruka-Kipro
Vijana wakiwa kwenye programu ya Ruka-Kipro

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TATIZO la ajira kwa vijana wengi hasa wanaomaliza vyuo vikuu hapa nchini, limeonekana kuongezeka. Ukubwa wa tatizo hili unachangiwa pia na wahitimu wengi kutokuwa na uzoefu wa kazi walizozisomea.

Tafati iliyofanywa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) mwaka 2011 imeonesha ni asilimia 10 tu ya wahitimu wanaomaliza vyuo vikuu hupata ajira rasmi, baadhi ya sababu zilizotajwa ni pamoja na ukosefu wa uzoefu kazini, matarajio makubwa ya wahitimu, pamoja na mitaala ya vyuo.

Waajiri wengi wanahitaji watu walio na uzoefu wa kazi na kiwango cha chini cha uzoefu mara nyingi huwa ni takriban miaka miwili, hivyo hali hiyo huwanyima nafasi wahitimu wengi kwenye fani mbalimbali hasa za masomo ya sanaa/ubunifu.

Kwa kutambua uwepo wa tatizo hilo na changamoto zingine za upatikanani wa uzoefu kwa wahitimu, ndipo Kampuni ya Ruka ilipoamua kuandaa programu maalumu ya kuwajengea uwezo na kuwapatia uzoefu vijana wenye vipaji pamoja na waliohitimu mafunzo vyuoni kupitia fani ya ubunifu kwa kutumia kompyuta.

Programu hii iliyopewa jina la Ruka-Kipro – lenye maana kuwa rukia uweledi inalenga kuwapa wahitimu uzoefu wa kazi wakati huo huo ikitoa fursa kwa wajasiriamali kufanyiwa kazi zao za ubunifu kwa kutumia kompyuta hasa kwa kusanifu vifungashio vya bidhaa zao pamoja na matangazo mbalimbali ili kutangaza bidhaa zao kwa lengo la kuongeza mauzo, kwani sote tunafahamu bidhaa inapotangazwa vizuri hujenga kuaminika kwa walaji.

Kwasasa tumeanza kwa majaribio kwa muda wa miezi mitatu vijana tuliowachagua kwa vigezo hasa wana nia ya kujifunza wanakuja hapa na kufanya kazi ikiwa ni sehemu ya kujifunza  kwa vitendo, wanakutanishwa na wataalamu ambao wana  wasimamia wakiwa  wanafanya kazi, kwasasa tumeanza na mashirika mawili ya  wajasirilamali kwa lengo la kuwajengea uzoefu,” anasema Mussa Sango ambaye ni Mwanzilishi wa programu hiyo.

Anasema mpango huo wa kuwajengea uzoefu wa kazi wahitimu ameuanzisha katika sekta ya kazi za ubunifu ambayo yeye alikuwa muathirika mkubwa wa suala la kukosa uzoefu hapo awali, pia anaona bado wahitimu wengi katika fani hizo wanakutana na kikwazo hicho cha uzoefu.

“Kwa bahati mbaya, kwa Watanzania nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo bado haitambuliwi kama ni sehemu maalumu ya kumpa mwanafuzi uzoefu wa kazi, lakini pia vijana hawana utamaduni wa kujitolewa kufanya kazi walizosomea ili kupata uzoefu sasa programu  hii inawapa fursa vijana kuja kujifunza kwa vitendo lakini watafanya kazi halisi za wajasiriamali na mashirika kama njia ya kuwatangaza na kuwapa ujuzi,” anasema Sango.

Anasema wahitimu hao wanachukuliwa kwa mfumo wa kujitolea ingawa huwezeshwa kwa kiasi kidogo cha nauli pamoja na chakula cha mchana, pia wanafanya kazi halisi za  kuonekana kulingana na fani ya ubunifu aliyobobea  wakati huo  akipata  maelekezo ya kitaalam kutoka kwa watu waliobobea kwenye fani husika.

Alisema aliamua kunzisha mradi huo baada ya kuona jinsi wahitimu wanavyoteseka na suala la  upatikanaji wa ajira hali ambayo inawafanya wengine kufanya kazi wasizozisomea ambapo kwa mujibu wa utafiri uliofanywa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) mwaka 2011, 90% ya wahitimu nchini Tanzania hawapati ajira kutokana na kukosa vigezo vya uzoefu wa kazi.

“Tunaamini kwamba mradi huu utawapa vijana uzoefu mzuri wa kazi, lakini pia kwa kuwa watakuwa wakifanya kazi halisi na kampuni/ mashirika, wajasiriamali  wadogo na wa kati pia tutakuwa tunawajengea mtandao mzuri utakaowawezesha  kupata ajira kutoka kwenye mashirika na kampuni mbalimbali,” anasema.

Anasema kwa sasa kutokana na uchanga wa mradi, wameanza na sekta ya ubinifu wa kazi mbalimbali ikiwamo mabango, matangazo, tofuti na kazi zingine ambapo wahitimu katika vyuo mbalimbali kwenye fani hizo watakaokuwa tayari wajiunga na programu ya Ruka-Kipro kwa malengo hayo yaliyokusudiwa.

“Tayari tumetoa mafunzo ya awali kwa vijana kumi na sasa tunao vijana wanne tunaofanya nao kazi kwenye kituo chetu cha Ruka-Kipro kilichowezeshwa na Shirika la Vijana la Music Mayday kwa kushirikiana na Shirika la Ubunifu la Ruka Tanzania, Kituo kipo eneo la wasanii maarufu Nafasi Art Space, Mikocheni B maeneo ya viwanda jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles