31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Rufiji watakiwa kutengeneza miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko

Na Mwandishi wetu-Rufiji

KUFUATIA miundombinu ya barabara, shule na zahanati kuathirika na mafuriko wilayani Rufiji, kamati za usimamizi wa maafa za wilaya hiyo, zimeshauriwa kuchukua hatua za haraka kwa kurejesha hali ya kawaida ya miundombinu iliyoathirika katika kata 13 za wilaya hiyo.

 Kata ya Muhoro na Chumbi ni miongoni mwa kata zilizoathirika sana na maafa hayo, ambapo kwa sasa madaraja matatu yaliyopo barabara ya Nyamwage – Utete inayoelekea makao makuu ya wilaya hiyo, tayari yameathirika.

 Daraja lililopo kwenye barabara ya kuelekea Mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere nalo limeathirika na Daraja la Mkapa nalo limeanza kupata athari ya mafuriko hayo.

Akizungumza baada ya kukagua athari za maafa  na kukabidhi misaada kwa waathirika, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, alielekeza kamati za usimamizi wa kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya, ziwajibike kutekeleza operesheni za dharura.

“Nimezishauri kamati za usimamizi wa  maafa katika wilaya hii kuwa na mipango ya muda mfupi ya kuhakikisha barabara zinapitika kipindi chote ili wananchi wasishindwe kutumia miundombinu hiyo.

“Zipo barabara zinaunganisha mikoa ya kusini na zipo barabara zinawasaidiia wananchi kuweza kuzifikia huduma za kijamii,”alisema Kanali Matamwe.

Awali Mkuu wa wa wilaya hiyo,  Juma Njwayo, alisema  misaada waliyopewa itakuwa ni msaada mkubwa kwa kuwa hadi sasa wapo watu zaidi ya 20,000 wameathirika na maafa hayo.

“Tunaishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutuletea magodoro, mikeka, vyandarua, ndoo na nabuni na naamini kamati za maafa zitawajibika kugawa vifaa hivi kwa mujibu wa taratibu za menejimenti ya maafa. Wilaya tunaendelea na kukabiliana  na maafa kwa kaya takribani elfu sita,  kama tulivyoshauriwa kuhusu miundombinu, kwa kushirikiana na TANROADS tunaendelea kwa kasi kuchukua hatua za kurejesha miundombinu yote iliyo athirika, ” alisema Njwayo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa, alisema tangu maafa ya mafuriko yatokee wilayani humo, wamekuwa wakipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa ofisi hiyo, kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu mwenye dhamana ya masuala ya maafa Jenista Mhagama, ambapo amekuwa akiwatuma wataalamu na kufika kwa wakati kwa ajili ya kuzisaidia kamati za usimamizi wa maafa.

“Wananchi wa Rufiji wanafarijika sana kwa jinsi Serikali yao inavyowajali, tunatambua mafuriko yamewaathiri sana ikiwemo na kuharibika kwa vyakula vyao, tunaomba  mtuletee mbegu ama chakula cha bei nafuu na wananchi hawataki chakula cha bure, sisi tunataka tufanye kazi na tukipata mbegu tutafanya kazi ya kilimo mara mafuriko yakiisha,” alisema Mchengerwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles