27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

RUFAA YA MBUNGE WA LONGIDO YATUPWA

 

 

 

Na JANETH MUSHI,
-ARUSHA


MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania,imeondoa kwa gharama rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Longido,Onesmo Ole Nangole (Chadema),dhidi ya aliyekuwa Mgombea wa Jimbo hilo kwa tiketi ya CCM,Dk. Steven Kiruswa, baada ya kushindwa kuzingatia amri ya mahakama hiyo iliyowataka kufanyia marekebisho rufaa hiyo.

Rufaa hiyo namba 129 ya mwaka 2016,Ole Nangole alikuwa anapinga uamuzi uliotolewa Juni 29, mwaka jana na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, uliomvua ubunge katika kesi ya uchaguzi namba 36 ya Mwaka 2015 iliyofunguliwa na Dk. Kiruswa.

Akisoma uamuzi huo, Msajili wa Mahakama ya Rufaa nchini, Amiri Msumi alisema baada ya jopo la majaji wanaosikuliza rufaa hiyo kupitia hoja za kisheria za pande zote mbili kwa kina wamebaini kwamba mawakili wa mleta rufaa wamekiuka maagizo ya mahakana ya rufaa yaliyowataka kufanya marekebisho na badala yake wakaongeza maneno yao na kuandika rufaa upya.

“Walipitia kamusi ili kupata za matoleo mbalimbali ili kupata tafsiri ya neno marekebisho 'amendement', ambapo inasema ni kurekebisha kasoro hivyo hawakupaswa kuandika upyaili rufaa hiyo," alisema Msajili.


Amesema kuwa amri ya mahakama ilikuwa ni kurekebisha rufaa hiyo na kuutaka upande wa Ole Nangole kuwaongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Longido kama wajibu rufaa wa pili na tatu ila badala yake wameandika rufaa upya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles