27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Rostam Aziz alivyochangia kuanzishwa NHIF

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ameweka wazi kuwa uamuzi wa kuwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ni mpango ulioasisiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz.

Katika kitabu chake cha ‘My Life, My Purpose’ alichokizindua wiki iliyopita jijiji Dar es Salaam, Mkapa ameeleza alijifunza mpango huo wakati mfanyabiashara huyo alipokuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga alikouasisi mwaka 1996 kabla ya kutangazwa rasmi kuwa wa kitaifa.

“Njia nyingine ya moja kwa moja ya kuwasaidia masikini ni kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ambao umejitolea kuzipatia familia hizo bima za afya.

“Nilijifunza kuhusu mpango huu kutoka kwa Rostam Aziz, Mbunge na mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa waliofanikiwa.
“Mwaka 1996 alianzisha mpango wa bima ya afya kwa wananchi wake wa Jimbo la Igunga kwa kiwango kidogo cha fedha ya Sh 10,000 ambacho kilisaidia familia yenye watoto wanne kutumia bima hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima. Tuliamua kuutangaza mpangohuu kitaifa,” ameeleza Mkapa katika kitabu chake hicho.

Amesema ingawa mpango huo ulipoanzishwa haukueleweka vizuri kwa watu kwani wengine walisema “sitaumwa sasa kwanini nitoe fedha yangu kwenye mfuko huu,” lakini waliendelea kusisitiza juu ya mpango huo.
Akielezea kuhusu magonjwa mbalimbali kama Virusi Vya Ukimwi (VVU), anasema ndani ya kipindi hicho serikali ilianza kupata hofu juu ya virusi vya ukimwi.

“Ugonjwa huu uligundulika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mwaka 1983 ambapo hadi kufikia mwaka 1986 kesi nyingi za ugonjwa huo ziliripotiwa.

“Mtangulizi wangu alianzisha programu maalumu ya kupambana na ugonjwa huo (National Aids Contol Programme), lakini tulikuwa tunahitaji bodi ya kushauri juu ya sera, utetezi, usimamizi na kusambaza taarifa.

“Nilianzisha Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini Tanzania inayotambulika kama Tacaids. Kujali kwangu juu ya madhara ya ugonjwa huu hatari usio na mwisho ulinipelekea kuanzisha Taasisi ya Benjamin William Mkapa baada ya kuondoka madarakani ambayo nitaielezea baadae,” anaeleza Mkapa katika kitabu hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles