30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rose Ndauka awapagawisha mashabiki Vikindu

Na Glory Mlay

MSANII wa filamu, Rose Ndauka aligeuka kivutio baada ya mashabiki waliojitokeza kuangalia mchezo wa fainali ya Swaiba Cup, kukacha mtanange huo na kujikuta wakimshangaa.

Mrembo huyo ambaye amewahi kutamba katika filamu mbalimbali za Kibongo, alitimba juzi Uwanja wa Ngunguti, Vikindu Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kuangalia fainali hiyo ya mpira wa miguu kati ya Ibdhu FC dhidi ya Toyo FC.

Katika fainali hiyo Toyo FC walitwaa taji hilo kwa mikwaju ya penalti 5-3 dhidi ya Ibdhu, lakini stori haikuwa ubingwa huo ni Rose Ndauka.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Rose Ndauka alisema amefarijika kuona vijana wanajituma katika michezo na kuwataka kutimiza malengo yao ya kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL).

Pia, aliwataka wanawake kufuata nyayo za mratibu, Asha Mbata kwa kuandaa michuano ya soka na kuanzisha vituo vya michezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles