24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

ROMA MKATOLIKI KUFUNDISHA SHULE YA MSINGI

Msanii wa muziki wa hip hop, Ibrahim Mussa (Roma Mkatoliki)

Na KYALAA SEHEYE,

KWA mara ya kwanza baada ya kutekwa na kuachiwa huru siku kadhaa zilizopita, msanii wa muziki wa hip hop, Ibrahim Mussa (Roma Mkatoliki), leo ameibukia shule ya msingi Mchikichini iliyopo Mbagala Rangi Tatu na kufundisha somo la hisabati kwa wanafunzi wa darasa la saba.

Msanii huyo mwenye taaluma ya ualimu, aliliambia MTANZANIA kwamba anafundisha somo hilo kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa sababu wanafunzi wengi hufeli somo hilo kutokana na uhaba wa walimu wa somo hilo.

“Mimi kitaaluma ni mwalimu wa hisabati, kutokana na kufeli mno somo hilo nimeamua kuanzisha kampeni ya kufundisha na kugawa vitabu kwa kuanza na shule hii kwa sababu pia nitakuja kufanya onyesho la muziki kwenye sikukuu ya Idd kwa mara ya kwanza,” alisema Roma.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ramadhani Juma, alithibitisha kwamba msanii huyo ameshapata kibali cha kufundisha shuleni kwake.

“Nimekagua na kugundua kuwa Roma ni mwalimu mzuri wa hisabati hivyo tumemkaribisha afundishe wanafunzi bila hofu, tukiwa na imani kubwa wataelewa kwa kuwa wanafundishwa na mtu wanayempenda na hii itaongeza morali ya wanafunzi shuleni hapa,” alisema mwalimu Juma.

Licha ya kufundisha pia atafuturisha watoto yatima wa kituo cha Nira kilichopo Mbagala Chamazi na atatoa zawadi za sikukuu ya Idd.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles