30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ROGER FEDERER AINGIA ROBO FAINALI US OPEN

NEW YORK, MAREKANI

BINGWA namba moja wa zamani wa mchezo wa tenisi, Roger Federer, amefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali kwenye michuano ya US Open, baada ya kumchapa mpinzani wake, Philipp Kohlschreiber.

Federer mwenye umri wa miaka 36 raia wa nchini Uswisi, alionesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo huo huku akiwa majeruhi, lakini aliweza kushinda kwa seti 6-4 6-2 7-5 dhidi ya mpinzani huyo.

Hii ni mara ya 12 kwa bingwa huyo kuweza kufika robo fainali kwenye michuano hiyo na anatarajia kukutana na mpinzani wake, Juan del Potro raia wa nchini Argentina. Wawili hao watakutana kwa mara ya pili huku mara ya kwanza ikiwa mwaka 2009.

Federer ambaye anashika nafasi ya tatu kwa ubora wa mchezo huo duniani, amesema anayo furaha kubwa kuweza kumshinda mpinzani wake ambaye anashika nafasi ya 28 kwa ubora.

“Mchezo ulikuwa mkubwa sana, mpinzani wangu alionesha ushindani wa hali ya juu, nilipambana kuhakikisha ninashinda japokuwa sikuwa sawa kiafya.

“Wakati ninaendelea na mchezo nilijikuta nikipata maumivu ya mgongo na ndio maana baada ya mchezo huo kumalizika, nilitoka haraka kwa ajili ya kumuona daktari, hali hiyo sikuweza kuionesha wakati nacheza nadhani ningempa nguvu zaidi mpinzani wangu.

“Ninayo furaha kuingia nafasi hii na ninaamini nitaweza kufanya vizuri zaidi kwenye mchezo ujao dhidi ya Juan del Potro, najua kila hatua ushindani wake unakuwa mkubwa zaidi, ila sina wasiwasi na mpinzani wangu japokuwa alinishinda 2009,” alisema Federer.

Kwa upande wa Kohlschreiber, amempongeza Federer kwa kumpa changamoto na anaamini mpinzani huyo anaweza kufanya vizuri zaidi.

“Federer ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa, lakini niliweza kupambana kwa kila namna ila nadhani mpinzani huyo alikuwa bora zaidi na kuna uwezekano akaendelea kufanya hivyo hatua inayofuata,” alisema Kohlschreiber.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles