25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Rodriguez afunguka Madrid

James RodriguezMadrid, Hispania

BAADA ya kukiongoza vema kikosi cha   Real Madrid, nyota wa timu hiyo, James Rodriguez, jana  alifunguka akidai anajifunza mengi kupitia kwa  kocha wake, Zinedine Zidane.

Rodriguez aliweka bayana mafanikio yake hasa baada ya juzi kuisaidia timu yake katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Espanyol.

Nyota huyo ambaye akuwahi kucheza tangu msimu uanze, alisaidia timu yake kuweka rekodi ya kushinda michezo 16 dhidi ya wapinzani wao katika michezo ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’.

Timu hiyo ilishinda mchezo huo  uliochezwa Uwanja  wa  Estadi Cornella-El Prat bila ya washambuliaji wake, nyota Cristiano Ronaldo na  Gareth Bale.

Mcolombia huyo anahaha  kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo licha kubainisha  kutokupangwa  katika kikosi hicho, anajifunza  vitu vingi kutoka kwa kocha wake.

“Zidane ni kocha ninayejifunza mambo mengi  kutoka kwake kwani kucheza timu hii ni ndoto yangu na  natumaini nitaendelea kufanya vizuri.

“Familia yangu kwa pamoja,  tuna furaha kuwapo hapa Madrid na kucheza kwenye timu hii, nitapambana nibaki hapa,” alisema.

Nyota huyo alisema si kweli yupo katika wakati mgumu ndani ya timu hiyo ingawa  mara kadhaa  hushindwa kuzungumzia hali hiyo mara kwa mara pindi anapoulizwa.

“Sisi tumejumuika kama timu  na kila mmoja wetu ana mchango katika timu hii tangu aliposajiliwa na klabu, hivyo tunahitaji kushinda zaidi ili tuweke rekodi nyingi.

“Ninaelewa  kuhusu maamuzi ya kocha, Zidane anaelewa kila wakati  nataka kuisaidia timu si  tu  kufunga na kusaidia bao lipatikane,” alisema  Rodriguez.

Nyota huyo alionesha kiwango kizuri katika mchezo huo kipindi cha kwanza na kusaidia vema na Karim Benzam aliyefunga bao la pili.

“Tulikuwa katika kiwango bora kipindi cha kwanza na  tulipambana kutafuta ushindi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles