25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Rio Ferdinand kupewa ukurugenzi United

MANCHESTER, ENGLAND 

BEKI wa kati wa zamani wa timu ya Manchester United, Rio Ferdinand, amethibitisha taarifa zinazosambaa kuwa anaweza kuja kuwa Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo siku za hivi karibuni.

Kwa mujibu wa BBC RM Sport, beki huyo ambaye alicheza katika kikosi cha timu hiyo kwa mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka 12, tayari amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa timu hiyo Ed Woodward kwa ajili ya kutaka kumpa nafasi hiyo.

Wamiliki wa timu hiyo kutoka familia ya Glazer, wameonesha nia ya wazi kutaka kumrudisha Ferdinand kwenye bodi ya timu hiyo ambaye alistaafu soka miaka minne iliopita.

Bila ya kujali kuwa kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa michezo kwenye kituo cha BT Sport, ameweka wazi kuwa, hatoweza kupata usingizi endapo atapata nafasi hiyo ndani ya Manchester United.

“Mwisho wa siku mimi ni binadamu, ninaamini kila mmoja anajua uhusiano wangu na Manchester United, upendo uliopo pande zote mbili.

“Endapo nitapewa nafasi hiyo ndani ya klabu kubwa kama ya Manchester United, bila shaka siwezi kukataa, lakini kwa sasa naomba niweke wazi kuwa, nina furaha na kazi yangu ya sasa, ninapenda kukaa kwenye kiti, napenda kuwa studio,” alisema Ferdinand.

Aliongeza kwa kusema, endapo atapata nafasi hiyo anaamini atakosa kabisa usingizi kwa kuwa atakuwa kwenye majukumu mazito kwa ajili ya klabu.

“Siku zote nimekuwa nikifanya mazungumzo na Ed Woodward tangu nilipoondoka United, hivyo ni wazi nipo kwenye uhusiano mkubwa na kiongozi huyo, sijakutana mara kwa mara lakini muda mwingi tunawasiliana kwa kutumia simu.

“Kila kitu kinawezekana na kama nitapata nafasi hiyo basi ninaamini sitoweza kulala kwa kuwa nitakuwa na majukumu mazito kwa ajili ya kuipigania timu,” aliongeza mchezaji huyo wa zamani raia wa nchini England.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles