RIHANNA AONYESHA UAMINIFU KWA ALEXANDER

0
425

BARBADOS, UINGEREZA              |                 


MWANAMUZIKI wa Uingereza anayetokea kisiwa cha Barbados, Robyn Rihanna, amedhihirisha kuwa umaarufu wake haujavunja urafiki wake wa utoto na Sonita Alexander.

Licha ya umaarufu huo, Rihanna (30), Jumamosi iliyopita alionekana katika harusi ya rafiki yake huyo iliyofanyika katika kisiwa cha Barbados.

Mwimbaji huyo alionekana mwenye furaha wakati wote wa sherehe za harusi hiyo, akiwa amevalia gauni refu lililokuwa na rangi ya bluu.

Rihanna ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Love On The Brain’, anadaiwa kuingiza kiasi cha dola milioni 100, baada ya siku 40 tangu wimbo huo kuachiwa Septemba mwaka jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here