RICH MAVOKO AFUNGUKA KUTOJIHUSISHA NA MITANDAO

0
148

Na JESSCA NANGAW


MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka lebo ya WCB, Richard Mavoko, amesema mara nyingi amekuwa akitumia muda wake mwingi kufikiria kutoa kazi nzuri zaidi badala ya kuingia kwenye mitandao ya kijamii zaidi kama ilivyo kwa wasanii wengine.

Mavoko amesema kutokana na hilo, anashukuru kuona kila nyimbo yake anayoitoa inapata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki wake na hiyo inatokana na kujipanga vyema kabla ya kutoa kazi zake.

Mavoko anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Rudi’ aliyomshirikisha msanii kutoka Nigeria Patoranking, amesema kujiweka ‘busy’ na kazi zake pamoja na ubunifu mpya kila kukicha, umekuwa ukiongeza chachu ya kufanya vizuri kwenye kazi zake.

“Nashukuru mapokezi ya kazi zangu ni makubwa na sijawahi kutoa nyimbo ikakosa kupendwa, nadhani utundu pamoja na ubunifu zaidi unazidi kuniinua kila siku, nimekuwa mara nyingi sipo kwenye mitandao ya kijamii na utanikuta nahangaika kujua nitoke vipi, kikubwa pia nadhani huu ni wakati wa kuupeleka muziki wangu kimataifa zaidi,” alisema Mavoko.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here