Refa atakayechezesha Simba na Yanga Septemba 30 ni Jonesia Rukyaa

0
1234

Na Elizabeth Joachim          |             


Shirikisho la mpira wa miguu Nchini (TFF) limemtangaza mwamuzi, Jonesia Rukyaa kutoka Kagera kuwa mwamuzi wa kati mechi ya watani wa jadi, Simba Sc ya Msimbazi na Yanga Sc ya Jangwani itakayopigwa Jumapili ya Septemba 30 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Jonesia atasaidiwa na mwamuzi Fednand Chacha kutoka Mwanza na Mohammed Mkono kutoka Tanga.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Septemba 26, Afisa Habari na Mawasiliano, Clifford Ndimbo amesema lengo la kutaja majina hayo ni ili waamuzi waweze kutambuana mapema kabla ya mchezo husika.

Ndimbo amesema katika mchezo huo utakaoanza majira ya Saa 10 jioni, muamuzi wa akiba atakuwa ni Elly Sasii kutoka Dar es salam na Kamishina wa mechi hiyo atakuwa John Komba kutoka Dodoma na mtathimini wa mchezo huo atakuwa ni Suddy Abdi kutoka Arusha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here