27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RC ASISITIZA UMUHIMU KUHIFADHI MAZINGIRA

NA SHOMARI BINDA

MKUU wa Mkoa wa Mara, Dk.Charles Mlingwa, amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kupambana na uhalribifu wa mazingira ikiwamo uhifadhi wa bonde la mto Mara   kuwafanya wanyama wanaovuka kupitia mto huo kuendelea kuvuka.

Katika miezi ya Aprili na Mei wanyama wakiwamo nyumbu, pundamilia na paa husafiri kutoka mbunga ya taifa Serengeti nchini   na kwenda mbuga za Masai Mara   Kenya kutafuta malisho na maji.

Wanyama hao hurudi  Tanzania miezi ya Julai na Oktoba kwa kutumia mto Mara, tukio ambalo huonekana kuwa ni muhimu na la historia.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kuelekea siku ya Mara ambayo huadhimishwa kila Septemba 15 kwa ushirikino wa  Tanzania na Kenya.   Mwaka huu maadhimisho hayo yatafanyika   wilayani Tarime.

 

RC alisema  wananchi wana umuhimu mkubwa wa kushirikishwa katika tukio hilo na uhifadhi wa mazingira.

Alisema umuhimu wa maadhimisho hayo ni kutoa msukumo mkubwa kwa hifadhi ya mto Mara ambao unaanzia katika milima ya Mau nchini Kenya na kuishia ziwa Victoria upande wa Tanzania

Mkuu huyo wa mkoa alisema mto Mara huchangia kwa kiwango kikubwa kuwapo   Hifadhi ya Serengeti ambayo ni tegemeo kubwa la pato la taifa na wananchi majirani na hifadhi kutokana na shughuli za utalii.

Alisema ili Hifadhi ya Serengeti iendelee kuwapo na  kutambulika katika maajabu saba ya Afrika kuhusu kuhama kwa wanyama, ni muhimu kuhifadhi mazingira ya bonde la Mto Mara na uhifadhi huo ni muhimu kushirikishwa   wananchi.

“Maadhimisho ya mwaka huu yatahusisha maonyesho na utoaji elimu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira ya bonde la mto Mara kwa   semina na makongamano, upandaji wa miti kwenye bonde, na haya yote wananchi wanapaswa kushirikishwa.

“Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu   ni “Afya ya Mto Mara kwa Maendeleo Endelevu”… lakini hatuwezi kuwa endelevu bila kuwashirikishwa wananchi katika utunzaji wa mazingira,”alisema.

RC alisema  serikali ya mkoa ilikwisha kupiga marufuku  wachenjuaji wa dhahabu   kufanya shughuli zao katika vyanzo vya maji katika mto Mara ili  kulinda mazingira yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles