28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

RC ASISITIZA KILIMO CHA ALIZETI TABORA

Na Tiganya Vincent, Maelezo

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ameagiza kuanzia msimu ujao wa kilimo kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi   alime heka mbili za alizeti.

Alisema hatua hiyo ni kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kujenga viwanda vya kusindika na kuzalisha mafuta hayo kuanza ujenzi mkoani humo.

Alitoa kauli hiyo kwenye maonyesho ya Nanenane Kanda ya Mikoa ya Magharibi yanayofanyika mkoani Tabora.

RC alisema alizeti mkoani Tabora inastawi na ikiwa wakazi wake watalima kwa wingi kampuni mbalimbali zitajitokeza kwa wingi kuja kujenga viwanda vya kuzalisha mafuta hayo.

Alisisitiza kuwa wawekezaji wengi wamekuwa wanashindwa   kujenga viwanda vya usindikaji wa mafuta hayo kwa sababu   zao hilo limekuwa halitiliwi mkazo na kufanya uzalishaji kuwa wa chini.

Mwanri alisema kwa sasa   itakuwa ajenda ya mkoa kama mkakati mojawapo wa kuwavutia watu kuja kujenga viwanda.

“Ndugu zangu wakuu wote wa wilaya na wakurugenzi kuanzia sasa akili yetu na agenda yetu kubwa iko katika kuhakikisha  kila mkazi wa Tabora analima  hekta mbili za alizeti kuanzia msimu ujao wa kilimo.

“Hii itatuwezesha tuwe na malighafi nyingi kwa ajili ya kulisha viwanda vitakavyoanzishwa kwa mwaka mzima.” Alisema.

Aliwaagiza maofisa ugani wote kuhakikisha wanawatembelea wakulima vijijini kuwaelimisha kilimo bora na mbegu bora za zao hilo.

RC alisema hatua hiyo itawawezesha wakulima kuanza  mara moja kilimo hicho   mvua ya masika itakapoanza.

Vilevile aliwaagiza wakurugenzi watendaji wote na maofisa ugani wote kuhakikisha   wanawahimiza wakazi wa maeneo mbalimbali ya mkoa huo kuanza kilimo cha   uwele, mtama, viazi na mihogo.

Alisema hatua hiyo ni katika kukabiliana na upungufu wa chakula kwa sababu ya mvua kuendelea kunyesha chini ya kiwango.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles