26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

RAY C AMTOLEA UVIVU NANDY

Na JENNIFER ULLEMBO

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amemtolea maneno  makali  mwimbaji Faustina Charles ‘Nandy’ na kumtaka kutotumia nyimbo zake anapopanda jukwaani kwenye matamasha yake mbalimbali.

Ray C alitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuandika ujumbe huo huku akimsisitiza Nandy kutumia nyimbo zake binafsi.

“Bado sijafa, kama watu wanaona umuhimu wa sauti yangu kwenye kazi mbalimbali ni vema nikaitwa mwenyewe na kushirikishwa, hii ni mara ya mwisho natoa onyo kwa Nandy,” aliandika Ray C.

Alisema kuwa hiyo si mara ya kwanza kwa Nandy kutumia nyimbo zake kinyume na maamuzi yake, hivyo ni bora kila mtu akafanya kazi zinazomhusu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles