28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

RAS Arusha avunja bodi kwa ufisadi

Na ELIYA MBONEA, ARUSHA

BODI na Menejimenti ya Chama cha Kuweka na Kukopa cha Kurugenzi Saccos iliyopo chini ya ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha, imevunjwa kwa tuhuma za ufisadi wa Sh milioni 600.

Aidha, Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika mkoani hapa, Nerei Kyara, ameagizwa kuchukua hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wanaokabiliwa na tuhuma hizo.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana mjini hapa na kusainiwa na Katibu Tawala, Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega, ilieleza kusimamishwa kazi mara moja kwa viongozi wa Kurugenzi Saccos.

Taarifa hiyo iliwataja waliosimamishwa kazi na kutakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria kuwa ni wakurugenzi wa bodi, Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Freedom Makiago, Meneja wa Saccos, Christine Sumaye na mejimenti yote.

“Kuanzia Agosti mosi mwaka huu, mrajisi wa vyama vya ushirika, Mkoa wa Arusha, uwe umechukua hatua na kumaliza mgogoro huu haraka, ikiwa ni pamoja na kuchukua taratibu zinazohusiana na sheria kuitisha mkutano mkuu maalumu wa wanachama wa Kurugenzi Saccos,” alisema Kwitega katika taarifa hiyo.

Alifafanua kuwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuwapo malalamiko mengi kutoka kwa wanachama wanaodai kutopatiwa mikopo kama ulivyo utaratibu.

“Kurugenzi Saccos inadaiwa mamilioni ya fedha kutoka kwa taasisi za fedha ikiwamo Benki ya CRDB na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambazo ziliikopesha Saccos hiyo,” alisema Kwitega.

Hivi karibuni, wanachama wa Kurugenzi Saccos walipokuwa kwenye mkutano mkuu maalumu, waliwasilisha maombi yao kwa Kwitega wakimwomba kuingilia kati tuhuma za ufisadi huo.

Walimwomba pia asitishe makato ya mishahara yao ambayo kwa miaka yote ilikuwa ikiendelea kukatwa ili kulipia mikopo kwenye Kurugenzi Saccos.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles