24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS WA ZAMANI WA IRAN AKBAR HASHEMI RAFSANJANI AFARIKI

president-akbar-hashemi-rafsanjani
Aliyekuwa Rais wa zamani wa Iran, Ayatollah Ali Akbar Hashemi Rafsanjani

Aliyekuwa Rais wa zamani wa Iran, Ayatollah Ali Akbar Hashemi Rafsanjani, afariki dunia jana huko mjini Tehran akiwa na umri wa miaka themanini na mbili.

Kifo chake kimetangazwa na Televisheni ya Taifa ya Iran huku ikitajwa kuwa, kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza kutoa salamu za rambirambi za kifo cha rais huyo mstaafu.

Licha ya tofauti walizokuwa nazo viongozi hao, lakini kiongozi huyo wa dini amemtaja Rafsanjani kama mpambanaji.

Rafsanjani alikuwa akimuunga mkono rais wa sasa Hassan Rouhani ambae amemsifu kuwa ni mwana mapinduzi mkubwa.

09rafsanjani3-master675
Kushoto ni Faezeh Hashemi Rafsanjani, mtoto wa marehemu Rafsanjani, akiwa na ndugu zake wakiomboleza.

Pamoja na mambo mengine, siku tatu za maombolezi zimetangazwa.

Ayatollah Rafsanjani aliwahi kuwa rais kati ya mwaka 1989 hadi 1997 na ameendelea kuwa na nafasi muhimu katika siasa za Iran.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles