24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS WA ERITREA KUZURU ETHIOPIA LEO

ADIS ABABA, ETHIOPIA


RAIS wa Eritrea, Isaias Afwerki, anatarajiwa kutembelea nchini Ethiopia leo, ikiwa ni siku chache baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri Mkuu Abiy Ahmed mjini Asmara.

Kwa mujibu wa Waziri wa Habari wa Eritrea, Yemane Meskel, ziara hiyo  itakuwa ya siku siku moja ambayo inategemewa kuongeza chachu katika mchakato wa amani ya kudumu na ushirikiano endelevu wa pande mbili.

Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, alitembelea mjini Asmara, nchini Eritrea na kukutana na Rais wa nchi hiyo, Isaias Afwerki, ambapo pande mbili zilitiliana saini mapatano ya kumaliza vita ambayo imekuwapo baina ya nchi hizo mbili kwa miongo miwili sasa.

Baada ya ziara hiyo, Abiy Ahmed alisema serikali yake iko tayari kutekeleza mapatano yaliyofikiwa ili kuwawezesha wananchi wa Ethiopia na Eritrea kupata fursa bora zaidi.

Eritrea ilijitenga na Ethiopia mwaka 1993 na kisha kukata uhusiano wa pande mbili na hivyo kupelekea Ethiopia ikose njia ya bahari.

KWA HABARI ZAIDI PATA NAKALA YAKO LA GAZETI LA MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles