27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS UFARANSA ASHIKILIWA KWA KUFADHILIWA KAMPENI


PARIS, UFARANSA

ALIYEKUWA Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, anashikiliwa na polisi, akihojiwa kuhusu tuhuma kwamba alipokea fedha za kufadhili kampeni zake kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi.

Polisi wanachunguza tuhuma hizo kuhusu ufadhili wa fedha alizotumia kwenye kampeni za uchaguzi wa urais mwaka 2007.

Msaidizi wake wa zamani, Alexandre Djouhri, pia alikamatwa London nchini Uingereza hivi karibuni.

Sarkozy, ambaye amekana tuhuma hizo, alishindwa katika jaribio na juhudi zake za kutaka kurejea madarakani mwaka 2012.

Duru kutoka kwa mahakama zimesema Sarkozy, aliyekuwa akijulikana kwa kupenda matanuzi, anahojiwa mjini Nanterre, magharibi mwa Paris.

Mwaka 2013, Ufaransa ilianzisha uchunguzi kuhusu tuhuma kuwa kampeni za Sarkozy zilipokea mchango kutoka hazina haramu za Gaddafi.

Duru zinasema mmoja wa mawaziri wa zamani wa Sarkozy na ambaye pia ni mshirika wake wa karibu, Brice Hortefeux, pia alihojiwa na polisi Jumanne iliyopita.

Tuhuma hizo zilitolewa na mfanyabiashara Mfaransa mwenye asili ya Lebanon, Ziad Takieddine na baadhi ya maofisa wa zamani wa Gaddafi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles