24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS TRUMP ‘AMPIGIA MAGOTI’ PUTIN

NEW YORK, Marekani 

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema kwamba, huenda akakutana na Kiongozi wa Urusi, Vladimir Putin, wakati wa ziara zake zitakazofanyika hivi karibuni katika eneo la Asia na Pacific.

Akizungumza jana katika mahojiano maalumu na jarida la FOX, Trump alisema kwamba, suala la kukutana na Rais Putin ni muhimu, kwa kile alichodai kwamba wanaweza kushirikiana kutafuta suluhisho  kuhusu mgogoro  Syria na Korea Kaskazini.

“Mbali na hayo, tukikutana tunaweza pia kuzungumzia jinsi hali ilivyo nchini Ukraine. Putin ni mtu muhimu sana kwa sababu anaweza kutusaidia  kuhusu ugomvi wetu na Korea Kaskazini,” alisema Trump.

Rais Trump anatarajia kuanza ziara ya siku tisa kesho katika nchi za Japan, Korea Kusini, China, Vietnam na Ufilipino, ambayo itakuwa ni ziara yake ya kwanza ya kikazi katika Bara la Asia, kabla ya Novemba 10 kuhudhuria mkutano wa nchi wanachama wa nchi za Ushirikiano wa Kiuchumi  Asia na Pasific (APEC), utakaofanyika nchini  Vietnam na mwingine wa Umoja wa nchi za Kusini mwa Asia (ASEAN) utakaofanyika mjini Manila, Ufilipino.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles