24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS PUTIN KUTOA TUZO

MOSCOW, URUSI


RAIS Vladimir Putin wa Urusi, anatarajia kutoa tuzo za kitaifa kwa waandishi, wanasayansi na wafanyakazi mashuhuri wa huduma za kibinadamu nchini humo, wakati wa maadhimisho ya siku ya Urusi, Juni 12 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania, utoaji wa tuzo hizo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Urusi, ambayo huadhimishwa tarehe hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa siku ya Urusi, raia wa taifa hilo huonesha fahari ya taifa lao huku baadhi wakisherehekea mafanikio ya kiuchumi na kijamii pamoja na kuwakumbuka watu maarufu na mashujaa wao.

Kwamba kwa vile siku hiyo ni mapumziko ya kitaifa kwa Shirikisho la Urusi, sehemu kubwa ya taasisi za kibenki, shule, ofisi za umma hufungwa na ikitokea siku kuangukia mwishoni mwa wiki husogezwa hadi Jumatatu.

Taarifa ilieleza zaidi kuwa Juni 12, 1990, viongozi wa uliokuwa Muungano wa Kisoshalisti wa Kisovieti wa Urusi (USSR), walitangaza azimio la taifa huru la Urusi. Waraka huo uliashiria mwanzo wa mageuzi ya kidemokrasia nchini humo.

“Pia iliashiria moja ya hatua za kwanza za kuvunjika rasmi kwa USSR baada ya yaliyokuwa majimbo mbalimbali kujiondoa katika muungano huo. Na miaka minne baadaye ikatangazwa rasmi kuwa siku ya mapumziko kitaifa.

“Kutokana na watu wengi kutoielewa au kukataa kuitambua, aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Boris Yeltsin aliitangaza kuwa siku ya Urusi mwaka 1997,” ilisomeka  taarifa hiyo.

Aidha, ilieleza zaidi kuwa pamoja na kupitishwa kisheria bungeni mwaa 2002, awali siku hiyo ambayo watu huadhimisha pamoja na mambo mengine, kwenda mapumziko (pikiniki), kushiriki matamasha na urushaji fataki, walikuwa hawaitambui au kuielewa.

“Kutokana na tarehe yake kuangukia wakati wa anguko la USSR, ambalo watu wanaona linakumbushia mateso ya kiuchumi na kijamii waliyokumbana nayo kipindi hicho, watu hawakuipenda, lakini sasa hali imebadilika,” tarifa hiyo ilisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles