25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS MAGUFULI KAULI ZAKO KUWA DARAJA LA WAPINZANI ?

Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

NA JAVIUS KAIJAGE,

DESEMBA 31 mwishoni mwa   mwaka jana, Rais John Magufuli akiwa katika mapumziko  yake mafupi, alitua  mkoani  Kagera ikiwa zimepita siku 112 tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi.

Akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo, Januari  2, mwaka huu  katika  viwanja vya shule ya Sekondari   ya Ihungo  mjini Bukoba, Rais  aliwahutubia mamia ya wananchi waliofurika kumsikiliza.

Katika hotuba yake iliyojaa  msisimuko, Mheshimiwa Rais aliwapa pole wakazi wa Kagera kwa kukumbwa na janga kubwa la tetemeko  ambalo lilipoteza maisha ya watu na mali  huku wengine wakijeruhiwa.

Pamoja na pole aliyotoa Mheshimiwa Rais  katika hotuba, vile vile aliendelea kusisitiza kuwa Serikali yake anayoiongoza haitaweza kutoa msaada kwa mtu mmoja mmoja mfano chakula au kujenga nyumba bali kitakachofanyika ni ujenzi wa miundombinu.

Mkuu huyo wa nchi akiwa anajinadi  kwa kusema ‘Msema kweli ni mpenzi wa Mungu’’ aliwahimiza Wanakagera kutobweteka bali wafanye kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo  huku akiwaamuru wasaidizi wake aliowateua kwa makusudi  hususani wanajeshi kuhakikisha  wanawawajibisha wananchi.

Kutokana  na  afya ya akili,  baada ya hotuba ile, baadhi ya watu wakiwamo wasomi, wanasiasa na wananchi wa kawaida wamekuwa wakiitafsiri katika  mitazamo tofauti.

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Bashiru Ally alisema kuwa katika mfumo wa siasa huru kuna  kutofautiana mitazamo kati ya wananchi, Serikali na viongozi wa siasa lakini ni wazi kuwa Rais alisimama katika msimamo wa Serikali yake na uwezo wa kutekeleza ahadi zake.

Kwa upande wake Dk. Benson Bana kutoka Chuo hicho cha Dar es Salaam alisema kuwa watu wanatafsiri vibaya maneno ya Mheshimiwa Rais aliyoyaongea mkoani Kagera hivi juzi. “Mheshimiwa ameongea ukweli kwa sababu ni sahihi kuwasaidia watu wengi kwa pamoja kuliko kumsaidia mtu mmoja mmoja,” alisema.

Naye Prof. Haji Semboja alisema kuwa kauli ya Rais ilikuwa ni kuwahimiza watu wa Kagera ambao  anajua wana uwezo wa mambo mengi ya kulima mazao mbalimbali kama vile  ya chakula na biashara  yanayoweza kuwapatia chakula cha kutosha.

Wakati wasomi hawa wakiwa na mitazamo hii, kwa upande wake Mwenyekiti  wa (Chadema), Freeman Mbowe ameikosoa hotuba ya  Rais Magufuli mkoani Kagera kwa kusema ” Hivi mtu ambaye amefiwa, nyumba imebomolewa, hana chakula, hana pesa unakwenda kutoa kauli za kibabe kwamba hutawapa chakula kwa kuwa Serikali haina shamba! hivyo si sawa sawa”

Mheshimiwa Mbowe akiwa kiongozi mkuu wa upinzani, kauli yake inaweza kuwa ya ukweli au ni namna ya kujitafutia umaarufu  ukizingatia katika siasa upinzani mara nyingi upo kwa lengo la kutaka kushika dola.

Katika awamu kadhaa zilizopita upinzani uliweza kuimarika kutokana na  matukio ya ufisadi. Nani hakumbuki kuwa Richmond ni miongoni mwa kashfa kubwa zilizoujenga upinzani hasa Chadema ?

Katika enzi hizi za ushindani kisiasa, chama makini  kama Chadema ikitokea kikakosa ajenda mahususi  za kuishitaki Serikali kwa wananchi kama inavyoonekana  sasa kwamba kutokana na uongozi wa JPM matukio ya ufisadi yanapungua kwa kasi, ni lazima utatafutwa udhaifu mwingine.

Ni kweli kiongozi anayetoa ahadi zinazotekelezeka ni  muungwana kuliko anayeahidi kukujengea ghorofa angani,  lakini kuna haja ya kuwa makini katika kauli maana  kutokana na ugumu wa maisha, wananchi wengi wanahitaji kujengwa kisakolojia kwa maneno ya hamasa   vinginevyo upinzani utatumia fursa  ya msongo wa mawazo yao kujinufaisha kisiasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles