30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS MAGUFULI ATOA ZAWADI ZA IDD ZENYE KUFIKIA SH MIL 10.9

Na LILIAN LUNDO – MAELEZO

RAIS John Pombe Magufuli ametoa zawadi za Idd El Fitri zenye thamani ya Sh 10,922,000 kwa vituo tisa vya Mkoa wa Dar es Salaam, vituo viwili vya Zanzibar na vituo 13 kutoka mikoa ya Tanzania Bara.

Zawadi hizo zilikabidhiwa jana katika Mahabusu ya Watoto iliyoko Upanga, Jijini Dar es Salaam na Kamishina Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Idara ya Ustawi wa Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Simon Panga, kwa niaba ya Rais.

Panga alizitaja zawadi zilizotolewa kuwa ni mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ambazo zinakusudiwa kuwezesha makundi hayo kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.

“Rais kwa upendo wake wa dhati ameona umuhimu wa kushiriki pamoja na watu walio katika makundi maalumu, wakiwamo watoto walio katika mazingira hatarishi na wazee wenye ulemavu wasiojiweza, wanaohudumiwa katika makazi, katika kusherehekea sikukuu ya Idd El Fitri mwaka 2017,” alisema Panga.

Alivitaja vituo vilivyonufaika na zawadi za Magufuli jijini Dar es Salaam kuwa ni Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini – Temeke, Makao ya Watoto IBN Kathry- Ilala, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Makao ya Watoto Yatima Chakuwama, Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund – Temeke, Makao ya Watoto Yatima Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization), Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam – Upanga, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Nunge – Kigamboni na Shule ya Ufundi ya Watoto Wenye Ulemavu Yombo.

Vituo vingine ni; Makao ya Watoto Tosamaganga – Iringa, Makao ya Watoto Yatima Malaika Kids Home, Mkuranga – Pwani, Makao ya Watoto Yatima Karibu Nyumbani, Kibaha – Pwani, Makao ya Watoto Yatima Miyuji Cheshire – Dodoma, Shule ya Maadilisho Irambo – Mbeya na Mahabusu ya Watoto – Mbeya.

Vituo vingine ni Mahabusu ya Watoto – Arusha, Makao ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto – Sinyanga, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ngehe – Ruvuma, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kiilima – Bukoba, Kagera, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Magugu – Manyara, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ipuli – Tabora, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Bukumbi – Mwanza.

Kwa upande wa Zanzibar, vituo vilivyonufaika ni Kituo cha Watoto Yatima Mabaoni – Chakechake – Pemba na Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Sebleni – Unguja.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles