31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Maduro awakaribisha wapinzani

ARAGUA, VENEZUELA

RAIS wa Venezuela, Nicolas Maduro, ameyakaribisha mazungumzo na upinzani yaliyoanza kufanyika huko nchini Norway, baada ya miezi kadhaa ya mapambano makali kati ya pande hizo mbili. 

Kwa mujibu wa tangazo lake alilotoa juzi mbele ya wanajeshi katika mji wa Aragua kuhusu kuanza kwa mazungumzo hayo, Rais Maduro amewataka raia nchini Venezuela kuyaunga mkono ili kufikia makubaliano ya amani na utulivu nchini humo. 

Maduro akiwa anakabiliwa na mgogoro mkubwa wa uchumi katika historia ya taifa hilo tajiri kwa mafuta, kiongozi huyo wa kisoshalisti amesema Venezuela inapaswa kushughulikia mizozo yake na kutafuta suluhisho kwa njia ya amani. 

Norway ilisema kupitia waziri wake wa mambo ya kigeni kuwa imefanikiwa kufanya mazungumzo ya awali na makundi muhimu ya kisiasa nchini Venezuela, bila kutoa maelezo ya ziada. 

Mazungumzo hayo ya amani yanafuatia miezi kadhaa ya mzozo wa kuwania madaraka kati ya Spika wa Bunge, Juan Guaido, aliyejitangaza kuwa rais wa mpito na Rais Maduro ambaye analaumiwa na jumuiya ya kimataifa kwa kulitumbukiza taifa hilo katika mgogoro wa kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles