31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS FIFA AAPA KUWASHUGHULIKIA MAFISADI

Na ASHA MUHAJI –DAR ES- SALAAM 

RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino, ameapa kutomwonea aibu kiongozi yeyote wa soka atakayebainika kutumia vibaya fedha za mpira.

“Katika utawala wangu ninapiga sana vita rushwa, nawahakikishia fedha ya mpira haitatumika vibaya, sitakubali kuona kiongozi yeyote anatumia vibaya fedha za mpira ikiwa ni sambamba na kupambana na vitendo vya rushwa,” alisema.

Infantino alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati akizungumza na baadhi ya wahariri wa michezo wa vyombo mbalimbali vya habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

“Mimi si rais wa ahadi bali ni wa kutenda, utawala wangu ni wa wazi kabisa kila kitu kinafanyika katika hali ya uwazi, hivyo sitarajii kuona mambo yakienda tofauti,” alisema.

Rais huyo alikuwa nchini kwa siku moja kuendesha mkutano wa siku moja kujadili maendeleo ya soka uliohudhuriwa na nchi 21 ambapo Tanzania ilikuwa ni mwenyeji wa mkutano huo.

Infantino ameahidi kufungua milango mipya ya mahusiano kati ya taasisi yake na TFF na kuanzia sasa ameahidi kuleta misaada tena baada ya kuwa ilisitisha hapo awali.

Alisema hatua hiyo inatokana na jitihada za wazi zinazofanywa na uongozi mpya wa TFF chini ya Wallace Karia ambaye ameonesha dhahiri kuendana na sera za wazi za taasisi yake.

“Tulisitisha misaada yetu kwa Tanzania lakini nimekuwa nikivutiwa na uongozi mpya wa TFF kwa jinsi wanavyojitahidi kutaka kuleta maendeleo, hivyo kuanzia sasa natamka kuwa tutaleta tena misaada yetu kwa TFF,” alisema.

Alisema jitihada hizo ndizo chanzo cha wao kuamua kuja nchini kufanya mkutano huo na kwa Tanzania hiyo ni mara yake ya kwanza kuandaa mkutano mkubwa kama huo. Mbali na Infantino, pia mkutano huo ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Fatma Samoura na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles