24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Bush kuzikwa alipozikwa mkewe

WASHINGTON DC, Marekani



RAIS  zamani wa nchi hii,  George HW Bush anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake Jimboni Texas katika eneo ambalo alizikwa mkewe,Barbra.

Kabla ya mazishi hayo ya leo jana viongozi kutoka mataifa mbalimbali walihudhuria ibada maalum ya kuuombea mwili wa kiongozi huyo iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Washington ambako ulipelekwa baada ya kuondolewa katika Jengo la Bunge la nchi hii.

Habari zilizopatikana mjini hapa zinaeleza kwamba miongoni mwa viongozi waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Rais  Donald Trump na watangulizi wake, Barack Obama, Bill Clinton na  Jimmy Carter.

Mbali na viongozi hao, taarifa hizo ziliwataja wengine kuwa ni  Prince wa  Wales, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel Mfalme na Jordan,  Abdullah II  na Waziri Mkuu wa zamani  John Major.

Kiongozi huyo ambaye aliitumikia nchini kama rais wa  41 kati ya mwaka  1989  na  1993, alifariki Ijumaa wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka  94.

Tangu alipofariki kumekwapo na shughuli mbalimbali za kuuaga mwili huo ambazo zilianza Jumatatu wiki hii kwa kuhamisha mwili huo kutoka Jimboni Texas hadi hapa kwa ajili ya kuwapa fursa viongozi na raia kuweza kutoka heshima hizo.

Jana pia ilikuwa ni siku ya maombolezo kitaifa ambapo ofisi nyingi za serikali zilifungwa likiwamo pia soko la hisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles