24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Bouteflika ajiuzulu

ALGIERS, ALGERIA

RAIS Abdelaziz Bouteflika amejiuzulu wadhifa wake baada ya miaka 20 kufuatia wiki kadhaa za maandamano ya kumpinga.

Jeshi la Algeria ambalo lina nguvu, lilimtaka kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kutangaza kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya uongozi.

Bouteflika amekuwa akionekana mara chache hadharani tangu agundulike kuwa na ugonjwa wa kiharusi miaka sita iliyopita.

Msukumo wa wananchi kutaka ajiuzulu ulianza kujijenga tangu Februari, na kusitisha tangazo lake la awali la kuwania tena urais.

“Rais wa Jamhuri, Abdelaziz Bouteflika ametangaza rasmi uamuzi wake wa kumaliza kazi yake kama Rais wa Jamhuri ya Algeria katika Baraza la Katiba. Uamuzi huo unaanza mara moja kuanzia leo,” taarifa iliyotangazwa katika televisheni ya taifa ilieleza jana.

Kuondoka madarakani kwa kiongozi huyo, pia kumekuja baada ya kiongozi wa maandamano kukataa ahadi aliyoitoa wiki hii kwamba atajiuzulu madarakani ifikapo Aprili 28.

 Waandamanaji wengi ambao ni vijana, wanadai kuwa wanataka mfumo mpya wa Serikali kutokana na kile wanachoona Bouteflika anatumika katika vikundi vya kisiasa, biashara na maofisa wa jeshi.

 Mamia ya watu wamesherehekea tangazo hilo katika mji mkuu wa Algiers, huku wakiwa wanapepea bendera ikiwa ishara ya furaha ya ushindi.

Selmaoui Seddik mmoja wa waliojitokeza barabarani kushangilia, alisema ingawa amepokea kwa furaha kujiuzulu kwa Rais Bouteflika, Serikali nzima inabidi pia iondoke.

 “Niko nje kusherehekea kujiuzulu kwa Rais Bouteflika. Tumeondoa kisiki madarakani. Kwa mapenzi ya Mungu, tutakuwa na asilimia 100 ya demokrasia ya mpito. Hilo ni jambo muhimu. Tunahitaji kuondoa utawala wote madarakani na hili ni jambo gumu.

“Ni vigumu kulifanya kwa amani, lakini nina imani na watu wa Algeria kulifanya kwa amani na kuelekea katika taasisi za uongozi na si magenge ya wahuni, kila kitu kitakuwa sawa. Mungu atasaidia,” alisema Selmaoui.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles