23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rais atangaza hali ya hatari

FREETOWN, SIERA LEONE

RAIS wa Sierra Leone, Julius Maada Bio, ametangaza vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa kingono kama hali ya hatari kwa taifa.

Tangazo hilo limetolewa juzi baada ya kuwepo malalamiko ya kushamiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa kingono nchini humo, ambako matukio ya ubakaji yameripotiwa kuongezeka mara mbili zaidi mwaka uliopita na kufikia 8,505 katika nchi hiyo yenye watu milioni 7.5.

Rais Bio amesema baadhi ya familia zinaendeleza utamaduni wa kukaa kimya na kutozungumza kuhusu unyanyasaji wa kingono, hali inayowaacha walengwa wakiwa wameathirika zaidi.

Bio ameongeza adhabu ya hadi kifungo cha maisha gerezani kwa watuhumiwa wa kesi za ubakaji wa watoto wadogo, kutoka adhabu ya kifungo cha miaka mitano gerezani hadi 15.

Takwimu za polisi zinaonesha kuwa theluthi moja ya visa vya ubakaji vilivyoripotiwa vinawahusisha watoto wadogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles