24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Raia wa kigeni wakamatwa na madini JNIA

Na Ruth Mnkeni, Dar es Salaam
RAIA wa kigeni wanaofanya biashara haramu ya madini wamekamatwa na madini yenye thamani ya Dola za Marekani 113,807.11 sawa Sh milioni 641.853 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TMAA, Bron Mteta alisema watu hao walikamatwa katika matukio 27 tofauti huku wakiwa na madini ya aina mbalimbali.
Alisema miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na lile la Juni 12 mwaka jana ambapo raia mmoja alikamatwa kwenye uwanja huo akiwa na madini ya vito vyenye uzito wa gramu 1,290 yenye thamani ya dola za Marekani 11,591.82.
Alisema mtuhumiwa alifikishwa mahakamani na kuhukumiwa adhabu ya kulipa faini ya Sh 300,000.
Alisema katika tukio jingine la Desemba 14 mwaka jana,raia mwingine wa kigeni alikamatwa kwenye uwanja huo akiwa na madini ya vito ya uzito wa karati 288 na thamani ya dola za Kimarekani 23,235.50.
Alisema mpaka sasa hatua za kisheria zimechukuliwa kwa mtuhumiwa huyo ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani na kupewa adhabu ya kulipa faini ya sh.500,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles