R. Kelly aombewa radhi na mwanawe

0
934

NEW YORK, MAREKANI

BAADA ya R. Kelly kukumbwa na kashfa ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya warembo nchini Marekani, mtoto wa staa huyo, Joann Kelly, ameamua kumuombea radhi baba yake.

Imefikia hatua sasa wasanii mbalimbali wanamtenga mkali huyo wa muziki wa RnB, kutokana na kashfa hiyo, hivyo Joann ameamua kufunguka kwa mara ya kwanza na kumuombea msamaha.

“Nianze kuomba radhi kwa ukimya wangu wa muda mrefu tangu habari hizi zienee, nawaombea kwa zile familia au wanawake ambao wamekuwa wakiguswa na kitendo cha baba yangu, ukweli ni kwamba hata mimi nimekuwa nikiumia kwa kipindi kirefu.

“Nimekuwa nikijua baba yangu ni nani, nimekulia hapo tangu nazaliwa, lakini nilichagua kukaa kimya kwa kile anachokifanya kwa ajili ya amani yangu, hivyo namuombea radhi baba yangu kwa yale yote yaliyotokea,” alisema Joann.

Baadhi ya wasanii kwa sasa wamefikia hatua kuwa na lengo la kufuta nyimbo ambazo wamefanya na msanii huyo na wengine wamedai hawana mpango kabisa wa kufanya naye kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here