PWC: SEKTA YA HOTELI AFRIKA INA FURSA ZAIDI

0
397
Hoteli ya kitalii Melia iliyopo kwenye mbuga maarufu ya utalii Serengeti mkoani Mara.
Hoteli ya kitalii Melia iliyopo kwenye mbuga maarufu ya utalii Serengeti mkoani Mara.

Na Mwandishi Wetu                  |                     


MAHOTELI ni kichocheo kikubwa cha biashara ya utalii kwa maana ya kutoa maeneo kwa usalama na uhakika ya malazi, burudani, mikutano,  huduma nyingine za biashara na maonyesho na kufanya kuwa ni kigezo muhimu cha mafanikio ya biashara hiyo.

Kwa dhana hiyo nchi nyingi zenye vivutio hafifu vya utalii zinafanya vizuri katika biashara ya utalii kutokana na kuwa na mahoteli  yenye sifa ya nyota nne na tano kwa wingi  na kuwa sumaku kubwa ya kuvutia wateja.

Mifano ni mingi ikiwamo Mauritius, Moroko na Kenya kwa Bara la Afrika.

Hivi basi utafiti wa kampuni ya mahesabu na uchumi, Price Waterhouse Coopers (PwC), inaonesha kuwa na imani kubwa na ukuaji wa biashara  ya mahoteli katika Afrika na hivyo kutabiri maongezeko makubwa ya fursa katika sekta hiyo ya uchumi kufuatana na ongezeko la mahitaji na utalii barani humu.

Ripoti ya PwC inaonesha  katika miaka mitano ijayo, mapato ya chumba cha hoteli ya Afrika Kusini yataongezeka zaidi na inatarajiwa  biashara kupanuka na kufikia  kiasi cha Randi bilioni 21.8 mwaka 2022, kwa ongezeko la hadi asilimia 5.6,  kila mwaka, kutoka kwa kiasi cha Randi bilioni 16.6 mwaka 2017. Randi ni fedha ya Afrika Kusini na moja inalingana na shilingi 320 za Tanzania.
Sekta ya hoteli ya Afrika ina uwezo wa kukua zaidi katika miaka mitano ijayo na hivyo kuongeza ajira kwa nchi hizo kwani sekta hiyo ya huduma huajiri watu wengi sana wa kuhudumu (labour intensive).

Kuongezeka kwa idadi ya wasafiri wa kigeni na wa ndani, pamoja na upanuzi katika minyororo kadhaa ya hoteli katika bara hili huimarisha uwezo wa sekta ya hoteli kupanua ukuaji wa biashara.

Hayo ni baadhi ya mambo muhimu kutoka kwa ripoti iliyotolewa  mwaka huu Julai 5, jijini Johanesburg na Kampuni ya PwC (www.PwC.com) kuhusu sekta ya hoteli ya Afrika; ikiwa ni toleo la 8 likibobea  zaidi kwenye mtazamo wa hoteli kwa muhula  wa 2018-2022  ikiainisha pamoja na habari kuhusu malazi ya hoteli nchini  Tanzania,  Afrika Kusini, Nigeria, Mauritius na Kenya.

Ripoti ya miradi ya mapato ya chumba cha hoteli kwa masoko matano hayo kama kikundi itaongezeka kwa asilimia 7.4 ya kila mwaka hadi kufikia Randi bilioni 50.5 mwaka 2022 kutoka Randi bilioni 35.2 mwaka jana.

Pietro Calicchio ni  Mkuu wa Sekta ya mahoteli wa  PwC  kwa Kusini mwa Afrika, anasema: “Utalii kwa Bara la Afrika umeonyesha kuwa imara katika kukabiliana na mambo mengi ikiwamo kutokuwa na uhakika wa kiuchumi na kisiasa, athari za ukame na mabadiliko mengine ya udhibiti. Fursa ni nyingi kwa sekta hii na kuonyesha  kufurahia ukuaji zaidi na hata kwa kasi zaidi. Hata hivyo, tunapoendelea kuchunguza tunaona pia kuna changamoto kadhaa zinazokabili kila nchi. Hii ni sekta ambayo inachukua hatua kwa mabadiliko hata madogo zaidi katika masuala ya kisiasa, udhibiti, usalama na uendelevu.” Yakikorofika kidogo tu mambo huwa tabu kwa waendeshaji na mlolongo mzima wa shughuli za ongezeko la thamani hasa utalii.

Mapato ya chumba cha hoteli ya Afrika Kusini yanatarajiwa kuongezeka hadi  Randi bilioni 21.8 mwaka 2022, kutoka kwa Randi bilioni 16.6 mwaka 2017.

Ukuaji wa  idadi ya vyumba vya hoteli nchini Afrika Kusini, unafanana na utabiri huo katika ‘Hoteli zetu 2017’ mtazamo wa ziada ya vyumba 2,900 kuongezwa zaidi ya miaka mitano ijayo.

Pia  PwC inatarajia viwango vya upangaji kuendelea kukua juu ya kipindi cha utabiri na kufikia 62.5% mwaka 2022.

Hivi sasa idadi ya wageni wa kimataifa kwa Afrika Kusini iliendelea kukua na ongezeko la 2.4% kwa jumla.

Mtazamo wa 2018 unabakia kuwa chanya kwa kiwango cha chini kuliko asilimia 2016.

Ripoti hiyo inasema kwamba, idadi ya wageni wa kigeni na utalii wa ndani itaongezeka kwa asilimia 5.3 mwaka 2018. Idadi ya wasafiri nchini Afrika Kusini inatarajiwa kufikia milioni 19.5 kwa  mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la kila mwaka la asilimia 4 kutoka kwa milioni 16 mwaka 2017. Takwimu  zimekuwa rahisi kupatikana kutoka Afrika Kusini  kuliko maeneo mengine kutokana na uwazi na uwezo wa kutoa takwimu kwa nchi hiyo na kutawaliwa na vikwazo katika nchi nyingine .

Suala la visa  (kibali) ni kikwazokwa ukuaji utalii Afrika Kusini na kwingineko na hasa Tanzania amabayo imektaa kuingia kwenye mpango wa visa moja kwenye eneo lote la Afrika Mashariki. Hivi sasa viasa moja hutumika kwa mafanikio  makubwa kama inavyodaoiwa na nchi za Kenya, Uganda na Rwanda. Tanzania ambayo ndio yenye vivutio vingi  imeona si sahihi kushiriki mpango huo kwani si salama na hauna vivutio kwake kuweza kushiriki kikamilifu  na hivyo kuomba ipewe muda zaidi.

“Kuna pia mjadala unaoendelea juu ya kupunguza mahitaji ya visa kwa wageni wa kimataifa kwani  hiyo inaweza kuathiri ukuaji wetu wa utabiri,” alisema  Calicchio akitoa maoni yake.

Taarifa  zinaonesha  kuwa  baada ya kupaa  kwa asilimia 38 mwaka 2016, wageni kutoka China kwenda Afrika Kusini walipungua kwa asilimia 17 mwaka jana, 2017.

Wakati huo huo wasafiri kutoka India waliongezeka kwa wastani wa  asilimia 2.7 mwaka 2017, ikiwa  chini ya asilimia 21.7 ya ongezeko la mwaka 2016.

Kwa nchi zisizo za Afrika, Uingereza bado chanzo kikubwa cha wageni Afrika Kusini na kufikia 447,901 mwaka 2017 na kuchangia ukuaji wa jumla wa asilimia 7.2 kwa wageni kutoka nchi zisizo za Kiafrika mwaka 2017.

Kwa wageni wa Afrika, idadi kubwa zaidi ilitoka Zimbabwe kwa kuingiza wageni milioni 2, ikifuatiwa na Lesotho kwa milioni 1.8 milioni na Msumbiji kwa milioni 1.3. Kuna mahusiano ya karibu ya kiuchumi na kijamii kwenye nchi hizo zinzounda Jumuia ya Uchumi  na Maendeleo Afika Kusini (SADC).
Siku za usoni
Ingawa msingi unaochochea utalii kwa Afrika Kusini unabaki mzuri, unaosaidiwa na kuboreka kwa  uchumi wa kimataifa na wa ndani, lakini kwa kiasi fulani unaathiriwa na mambo mengine kama uhaba wa maji huko Cape Town.

Kama kuna utabiri mdogo wa kihistoria, ni vigumu  kusema  kwani mradi wa athari za ukame juu ya utalii ni jambo jipya na hivyo kufanya  makisio ni kuwa tusubiri na tutazame (wait and see).

Suala li wazi kwa kuangalia  mahitaji  ya nafasi (booking) yalikuwa  chini kwa Cape Town, na kwa vile utalii wa jumla wa Afrika Kusini hufanyika  wakati wa msimu wa sherehe  (mwishoni  mwa mwaka) na kwa kweli ulichukua nafasi  kubwa katika robo ya kwanza ya 2018.

Hoteli katika Cape Town wanachukua hatua kadhaa za kuhifadhi maji. Ikiwa mvua ya baridi inaendelea kwa kiwango cha sasa, mgogoro unaweza kuwa mdogo katika fani.

Nigeria inatarajiwa kuwa nchi inayoongeza kwa kasi zaidi mahoteli katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Hoteli kadhaa mpya zimepangwa kufunguliwa wakati huu. Uboreshaji unaoendelea katika uchumi wa ndani utaongoza pia ukuaji wa haraka  wa matumizi kwa siku kwa wageni.
Kenya, Tanzania na Mauritius inapaswa kukua kwa haraka zaidi, pamoja na ongezeko la kila mwaka la  asilimia 9,  9.1 na 7.2, kwa mtiririko huo. Afrika Kusini inaelekezwa kuwa soko lenye kasi zaidi na kuongezeka kwa asilimia 5.6 ya kila mwaka katika mapato ya chumba.

Malazi ya hoteli

Katika nchi za Afrika Kusini, Nigeria, Mauritius, Kenya, Tanzania  yanapambwa na mafanikio thabiti.
Kwa ujumla, ukazi wa chumba  na mapato ya hoteli   nyota tano nchini Afrika Kusini yaliongezeka kwa asilimia 4.6 hadi kufikia bilioni R16.6 mwaka 2017. Hoteli za nyota tano zilikuwa na viwango vya juu zaidi vya ukazi (ocupancy) katika soko mwaka 2017, kwa asilimia 79.5.

Wakati ukuaji wa kiwango cha wastani wa tozo kila siku (ADR) kwa hoteli ya nyota tano ulipungua kwa  mwaka 2017 (R 2,6 milioni), kama ulivyofanya kwa soko kwa ujumla, kwa ongezeko la asilimia  8.8 lilikuwa limeongezeka sana kwa ongezeko la hoteli ya nyota tatu na nne, kuonyesha athari za kiwango cha juu cha ukazi  kwa hoteli nyota tano.

Pamoja na hoteli kadhaa za nyota nne zilizofunguliwa mwaka 2017, vyumba vilivyopo vimeongezeka  kwa asilimia 1.8 na hivyo kupanda kwa mara ya kwanza tangu 2013.

Nyingi  ya fursa za hoteli iliyopangwa kwa miaka ijayo itakuwa ni kwa hoteli za nyota nne, na kusababisha kuongezeka kwa asilimia 2.4 kila mwaka.

Mahoteli Tanzania

Wakati huo huo biashara ya mahoteli nchini Tanzania inaonekana kupungua  wateja baada ya Serikali kuwa na sera tofauti ya awali na kuanza kutotumia mahoteli kwa kuendesha semina zake  na hivyo kutumia kumbi za taasisi zake. Hoteli nchini zimeathirika kwa kutegemea watalii pekee ambao kawa kawaida ni biashara ya msimu na kufanya hpteli zionekane kama mahame.

Hayo yaliibuka kwenye mkutano wa serikali na wadau  wenye mahoteli.

Serikali  ilisimaia maamuzi yake na kutoa ushauri  kwa kuwataka wamiliki wa vitegauchumi hivyo kuwa wabunifu kwa kuwekeza nje ya miji ya Dar es Salaam na Arusha ili kutumia fursa mbalimbali kwa ajili ya soko la utalii na hoteli barani Afrika linalokua.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, alisema njia za kuingiza pesa katika hoteli ni nyingi  sana na aghalabu hutegemea  serikali. Aliwa aambia  wajumbe kwamba kinachotakiwa ni ubunifu pamoja na kuitisha mikutano mbalimbali, ikiwemo ya kimataifa, ambayo itawezesha kuliingizia taifa kipato alisema  hayo jijini Dar es Salaam  hivi karibuni.

Alisema katika mkutano mkuu wa awamu ya nne wa hoteli za Afrika kuwa Tanzania kuna hoteli takribani 385 ukiachia za Zanzibar,  zenye hadhi ya kupokea watalii, lakini changamoto iliyopo ni kwamba hoteli nyingi zipo katika majiji ya Arusha, 172  na Dar es Salaam, ambayo ina hoteli 291.

Aliwaomba wawekezaji kutumia fursa hiyo kuwekeza kwa kujenga hoteli katika maeneo mbalimbali ya mikoa mingine kwani vivutio vimesambaa kote nchini.

“Kwa mfano Mkoa wa Lindi na Mtwara ambako kuna ugunduzi wa gesi wawekezaji wanaweza kujenga mahoteli kule badala ya kutegemea hizi zilizopo Dar es Salaam,” alisema Meja Jenerali  Milanzi.

Alisema utalii unaliingizia Taifa mapato kwa asilimia 17 na kwamba kama utaendelezwa vizuri mapato yataongezeka zaidi ya hapo na kuweza kufikia lengo la serikali la kuifanya  nchi  kuwa ya viwanda.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania, Richard Rugimbana, alisema mkutano huo unalenga kulinganisha maendeleo ya hoteli katika nchi za Afrika, ikiwa ni pamoja na kupata taarifa za maendeleo yake na changamoto inazozikabili.

Alisema taarifa iliyotolewa katika mkutano huo inasema dunia nzima, Afrika inapata watalii asilimia 5 na ile asilimia 95 wanakwenda Marekani, bara la Ulaya na bara la Asia.

Alisema utalii wa Tanzania unakuwa na changamoto kutokana na kutokuwa na matangazo ya kutosha, ikiwa ni pamoja na miundombinu mibovu.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya LNoppen Group, alisema wamefanya mkutano huo nchini kutokana na fursa zilizopo, hasa katika sekta ya ukarimu na utalii.

Mahoteli ya haja nchini

Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kwa  biashara ya utalii wa safari kutokana na kuwa na vivutio vingi ikiwamo Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya Serengeti, Bonde la Ngorongoro  ikiwa vivutio vitatu vikuu Afrika kati ya maajabu saba. Visiwa vya viungo Zanzibar ni eneo lingine lililosheheni vivutio lukuki  na utamaduni uliotukuka wa miaka mingi.

Tanzania ina sehemu kubwa tatu za utalii huo ikiongozwa na Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar na juhudi inafanywa kufungua ushoroba wa Kusini utakaokuwa na makao makuu yake Iringa.

Miundombinu inaboreshwa ikiwamo mahoteli, viwanja vya ndege na barabara ili kufanya utalii ushamiri kote Kaskazini  na Kusini kwani kuna vivutio tosha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here