25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

PUTIN AWAACHA MBALI WAPINZANI WAKE KURA ZA MAONI

MOSCOW, Urusi


RAIS wa Urusi, Vladimir Putin ameendelea kuongoza katika kura za maoni baada ya utafiti mwingine kumpatia asilimia 81 ya wapiga kura waliopanga kujitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao.

Utafiti huo ambao ulitolewa juzi na Kituo Cha Utafiti cha Taifa ulionesha idadi hiyo ni pungufu ya asilimia 2.7 ya ile ya Desemba 17 mwaka jana.

Katika matokeo ya utafiti huo wagombea wengine walionekana kuachwa mbali na kiongozi huyo, ambapo mgombea wa Chama Cha Kikomunisti, Pavel Grudinin aliambulia asilimia  7.6 huku Gennady Zyuganov wa chama cha CPRF akiambulia asilimia  3.3 kama aliyopata mwezi uliopita.

Katika matokeo hayo kiongozi wa Chama Cha  LDPR, Vladimir Zhirinovsky aliongeza asilimia 0.1 katika idadi aliyoipata mwezi uliopita na hivyo kuwa watatu nyuma ya Rais  Putin  na  Grudinin akipata asilimia 4.2  ya kura hizo.

Kwa upande wake Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni,  Ksenia Sobchak alipata asilimia  0.7 kutoka asilimia 0.3  ya aliyoipata mwezi uliopota.

Kwa mujibu wa utafiti huo asilimia 0.4 walihojiwa walisema watampigia kura kiongozi wa Chama Cha  Growth, Boris Titov idadi ambayo ni pungufu ya asilimia  0.2 ya aliyopata Desemba 17 mwaka jana.

Na asilimia 0.6 wakisema kuwa watawapigia kura wagombea wengine wakati asilimia  4.4 wakisema kuwa bado hawajaamua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles