30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

PUTIN AFUNGUKA MGOGORO WA KOREA KASKAZINI

MOSCOW, Urusi

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, ametoa ushauri kuhusu mgogoro wa Korea Kaskazini na Korea Kusini akisema kwamba unaweza kutatuliwa kwa njia ya majadiliano na wala si kwa kivita.

Putin amesema hayo juzi wakati akiwahutubia wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Valdai  na akapinga kuhusu vita dhidi ya Korea Kaskazini na akashauri kwamba nchi hiyo ni bora  kushirikiana nayo katika miradi mbalimbali ili kupunguza mvutano na Korea Kusini.

Katika hotuba hiyo Rais Putin alisema vikwazo dhidi ya  Korea Kaskazini haviwezi kusaidia kitu chochote bali utaongeza zaidi  migongano baina ya pande hizo mbili.

“Hali ni ya hatari. Ni nani anayeweza kusema ni kitu gani  Korea Kaskazini wanacho na wanaficha wapi  na kama ikiwekewa vikwazo itaharibu kila kitu. Kwanini tunakuwa na chaguo moja, inabidi tuwe na makubaliano  na kuiheshimu nchi,” alisema Rais Putin.

Rais huyo alikwenda mbali zaidi  akisema kama vikwazo vingekuwa njia mbadala basi yale makubaliano ya awali Serikali ya Pyongyang isingekuwa na mafanikio. Amesema Urusi tayari imesambaza miradi kadhaa na pia kwamba inahusisha Korea ya Kaskazini na Kusini katika miradi ya mabomba na  ujenzi wa reli na mabomba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles