27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA NDULLU AALIKWA TAKWIMU

Na JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, anatarajiwa kushiriki kutathimini programu ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano (FYDP-II) na Agenda ya Dunia ya mwaka 2030 ya Malengo Endelevu (SDGs).

Tathimini hiyo inatarajiwa kufanyika Novemba 20 ambayo pia ni siku ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika.

Akizungumza jijini hapa jana, mkurugenzi wa shughuli za Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Erenius Ruyobya alisema maadhimisho hayo yana lengo la kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa tasnia hiyo katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.

“Kauli mbiu ya siku hiyo kwa mwaka huu ni ‘Takwimu bora za uchumi kwa maisha bora’ inayolenga kuweka mkazo katika matumizi ya Takwimu za uchumi kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wote na Afrika kwa ujumla.

“Kwa mantiki ya matumizi sahihi ya Takwimu za uchumi yanawezesha Serikali kutunga sera na kutathimini programu mbalimbali kama vile Agenda ya Afrika ya Mwaka 2063,” alisema Ruyobya.

Alisema programu hizo zina lengo la kuboresha maisha ya wananchi kwa kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa Huduma za afya, Elimu, Miundombinu, Mwasiliano, Utunzaji wa mazingira pamoja na Utawala bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles