27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Ndalichako ataka tafiti za viwanda

Profesa Joyce NdalichakoMAULI MUYENJWA NA BETHA MWAMBALASWA (MSPS), DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ameagiza tafiti zinazofanywa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) zilenge katika viwanda ili kuongeza kasi kuelekea uchumi wa viwanda.

Akizindua kongamano la tano la teknolojia na ubunifu jana Jijini Dar es Salaam, alisema serikali imeweka dhamira katika viwanda, ubunifu na utafiti, vikiunganishwa vitaleta mapinduzi ya viwanda nchini.

“Lengo kuu la tafiti hizi ni ili zitoe matokeo ambayo yanagusa maisha ya wananchi, hasa wa maisha ya chini na katika shughuli zao za kiuchumi.

“Nimeambiwa Taasisi ya Jeshi ya Mzinga wametengeneza breki za treni kwa ajili ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) ambazo zilikuwa zinanunuliwa nje na pia nimeambiwa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) wamegundua chanjo ya kuku ya magonjwa mbalimbali.

“Wahakikishe chanjo hiyo inasambazwa nchi nzima, itasaidia kutatua tatizo la mifugo ya kuku kufa kwa magonjwa mbalimbali na wafanyabiashara wengi watanufaika, nikiwemo mimi mwenyewe kwa kuwa nafuga kuku pia,” alisema Profesa Ndalichako.

Ndalichako alisema mfano wa matokeo mazuri ya tafiti ambazo zimeshafanywa ni pamoja na tafiti za SUA, ambacho kimeweza kugundua mbegu za mahindi, mpunga na mihogo ambazo zinaweza kustahimili ukame kwa muda mrefu na kupambana na magonjwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa COSTECH, Dk. Hassan Mshinda, alisema ili kufikia malengo ya mapinduzi ya viwanda kama serikali ya awamu ya tano inavyotaka, ni lazima kuwekeza katika utafiti na ubunifu katika maendeleo ya viwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles