27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA MAGHEMBE ASISITIZA KILIMO CHA KISASA

Na Mwandishi Wetu

-Morogoro



WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amewashauri wakulima kufanya kilimo cha kisayansi na teknolojia ili kuongeza mavuno na kupata kipato zaidi.

Akizungumza katika maonyesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro jana, Profesa Maghembe alisema maofisa wa Serikali wanaohusika na kilimo wawasimamie wakulima ili kupata tija na kuondokana na kilimo cha kimazoea.

“Lazima wakulima wasimamiwe, wafuatishe mambo ya kisayansi na teknolojia kwenye kilimo, wapate pembejeo na viatilifu vya kisasa na zana za kupandia zisizopoteza mbegu au kuziharibu.

“Si sahihi mtu kulima ekari 200 halafu apate magunia 200, si sahihi hata kidogo. Tunataka wakulima wavune mazao mengi kulingana na nguvu waliyowekeza wakati wa kuandaa shamba na kupanda. Hili litawaongezea ushawishi wa kulima zaidi,” alisema Profesa Maghembe.

Akizungumzia kuhusu teknolojia ya uhandisi jeni ambayo inazalisha mazao au viumbe vilivyobadilishwa vinasaba (GMO’s), Profesa Maghembe alisema teknolojia hiyo ni muhimu ikafundishwa kwa wakulima na wataalamu wa kilimo ngazi zote.

“Yapo mambo ya msingi hapa, katika miaka hii tunayokwenda katika uchumi wa kati lazima tutumie mazao ya GMO kwa yale mazao yanayopasa kufanya hivyo, ni kichocheo cha kuwafanya wakulima wazalishe na kupata bei  nzuri zaidi.

“Wenzangu wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa wilaya, jambo la kwanza lazima tuondoke katika kilimo cha kimazoea na kuhakikisha wakulima hawalanguliwi, wakati wakulima wakishavuna wanakuwa wamechoka, wanahitaji chakula na kupeleka watoto shule, hapo ndipo wanunuzi wanakwenda kuwalangua, lakini wanawalangua kitu gani kwa sababu hata faida yenyewe hawajapata,” alisema.

Kuhusu suala la bei, Profesa Maghembe ambaye katika awamu ya nne alikuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, aliishauri Serikali iweke bei ya mazao kulingana na bei ya kidunia.

“Ni muhimu tutoe rai hapa, lile soko la mazao lianzishwe mara moja ili kila kitu kifanyike hapahapa, nina uhakika walanguzi hawatakuja

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles