29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Kabudi: Hakuna Mtanzania aliyepata virusi vya corona China

Mwandishi Wetu -Dar es Salam


WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, amesema kuwa hadi sasa hakuna Mtanzania yeyote aliyeathiriwa ama kukumbwa na virusi vya homa ya corona nchini China.

Profesa Kabudi aliyasema hayo jana Dar es Salaam, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu hali ya Watanzania waishio China kutokana na kuzuka kwa virusi vya ugonjwa huo nchini humo.

Alisema Tanzania ina wanafunzi takribani 4,000 ambapo katika mji wa Wuhan kuna wanafunzi 400 na kwamba Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki ameihakikishia Serikali kuwa hadi sasa hakuna Mtanzania yeyote aliyeathiriwa ama kukumbwa na maradhi hayo.

Aliongeza kuwa Tanzania inaendelea kufuatilia kwa ukaribu kujua maendeleo na hali za Watanzania wanaoishi jimboni Wuhan na China kwa ujumla.

Profesa Kabudi aliwataka Watanzania kuwa watulivu, makini na kupenda kuwa na subira ya kupata maelezo, maelekezo na ufafanuzi rasmi wa Serikali pale kunapotokea jambo badala ya kukimbilia kwenye mitandao na uvumi.

Aidha amewataka Watanzania kuwa makini na suala la kutoa taarifa zisizo rasmi ama uvumi kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles