25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA KABUDI AMWOKOA WAZIRI ANGELA KAIRUKI

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, amekamilisha kanuni za sheria ya madini namba 7 ya mwaka 2017 na kuwasilisha vitabu vya kanuni hizo kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.

Ni wazi hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli, alilomtaka Waziri wa Madini, Angellah Kairuki kwa kushirikiana na gulu huyo wa sheria kuhakikisha wanasaini kanuni hizo hadi kufikia leo.

Profesa Kabudi, aliwasilisha kanuni hizo Ikulu Dar es Salaam, akiwa na naibu mawaziri wa madini, Stanslaus Nyongo na Doto Biteko.

Alisema kanuni hizo zimekamilika siku moja kabla ya tarehe ya mwisho iliyotolewa na Rais Magufuli na kubainisha kuwa sasa sheria inaweza kuanza kutumika.

Kwa upande wao, naibu mawaziri hao, wamewataka Watanzania na wadau wote wa sekta ya madini kushirikiana na Serikali kutekeleza sheria hiyo na wamempongeza Rais Magufuli kwa kutoa msukumo wa kukamilishwa kwa kanuni hizo.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amepokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Novemba 25, mwaka jana wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi (Mloganzila) kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Baadhi ya maagizo hayo ni kupunguza baadhi ya idara na madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuhamishia Mloganzila na hospitali za mikoa kuhamishwa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Ummy alisema amewasilisha taarifa hiyo akiwa ameongozana na viongozi wakuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKHI) na Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi (MUHAS).

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles