31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Ndalichako kufungua maonyesho ya sayansi

Christina Gauluhanga -Dar es salaam

MAONYESHO ya tisa ya kitaifa ya sayansi na teknolojia ya shule za sekondari, yanatarajiwa kufanyika kesho Julai 31, hadi Agosti Mosi, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST), Profesa Yunus Mgaya, alisema mgeni rasmi katika maonyesho hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

Alisema maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka, kwa mwaka huu kazi za sayansi na teknolojia zilizotafitiwa na wanafunzi 190 chini ya walimu wao zitaonyeshwa.

Alisema wanafunzi watakaoshiriki maonyesho hayo Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere watapata fursa ya kuboresha ujuzi wao wa kisayansi kupitia mpango wa uwezeshaji ulioendeshwa na wanasayansi washauri wa YST uliorabitiwa na waratibu wa mikoa ya YST.

“Mpango huu wa kuzitembelea shule na kutoa mafunzo ya kisayansi kwa walimu na wanafunzi umekuwa muhimu kwa wanaowezeshwa na ufadhili endelevu wa wafadhili wetu wakuu Karimjee Jivanjee Foundation na Shell Exploration and Production Tanzania,” alisema Profesa Mgaya.

Alisema pia kuna wadhamini wengine wa tasnia ya sayansi kama Ukaid, Serikali ya Ujerumani kupitia Siemens Tanzania, Songas Ltd na Institute of Physics.

“Pia tunawasikiliza Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kwani ni fursa kwa wanafunzi kuonyesha tafiti zao ambazo zinachangia kutatua tatizo za kijamii pamoja na kujionea udadisi wa vijana wetu,” alisema Profesa Mgaya.

Alisema kwa siku mbili za maonyesho wanasayansi chipukizi wataonyesha kazi zao katika nyanja mbalimbali za sayansi ikiwamo kemia, fizikia, hesabu, biolojia, mazingira, sayansi ya jamii na teknolojia.

Alisema awali shule 144 zilishiriki kufanya utafiti Januari hadi Februari mwaka huu ambapo kulikuwa pia na waratibu 27 nchi nzima, waliopewa mafunzo.

Kwa upande wake, mwazilishi mwenza wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha, alisema maonyesho haya ambayo yanatoa fursa kwa wanafunzi kuonyesha ugunduzi wao yanafanyika kwa mara ya tisa sasa.

Aliiomba jamii kuwaunga mkono wanasayansi chipukizi ili waweze kufikia malengo yao ya kisayansi.

Alisema ifike wakati sasa jamii kuona haja ya kufanya mabadiliko kwa masomo ya sayansi yawe ya vitendo ili miradi inayobuniwa iwe na faida kwa jamii.

“Mpango huu utasaidia kuamsha ari ya wanafunzi kusoma masomo ya sayansi na kuboresha ufaulu zaidi kwa wanafunzi,” alisema Kamugisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles