33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

PROF. NDALICHAKO AWAPA SOMO WANAFUNZI PWANI

NA MWANDISHI WETU

-MKURANGA

WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako,  amewataka wanafunzi wa shule za sekondari Mwinyi na Nasibugani kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwa kuacha kujiingiza kwenye vikundi au mambo ambayo hayana tija kwa maendeleo ya Taifa.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo jana wakati alipofanya ziara wilayani Mkuranga mkoani Pwani, kwa lengo la kukagua ujenzi unaoendelea wa vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo katika shule hizo ambao unatekelezwa na  programu ya Lipa kulingana na matokeo.

Profesa Ndalichako alisema jitihada zinazofanywa na Rais John Magufuli za kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi zinapaswa kuungwa mkono kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo, ikiwa ni pamoja na wanafunzi kufaulu vizuri.

Waziri Ndalichako amesisitiza kuwa Serikali haihitaji kuona wanafunzi wanafeli bali  inataka kuona wanafunzi wanafaulu ambapo  amewasihi walimu kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia weledi.

Naye Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (CCM), alimshukuru Waziri Ndalichako kwa kutatua kwa wakati changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles