25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Prince William kukutana na Rais Magufuli

LONDON, UINGEREZA
Mwanamfalme wa Uingereza William anapangiwa kukutana na Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli wakati wa ziara yake ya siku saba barani Afrika.

Anatarajiwa kuzuru pia Kenya na Namibia katika ziara hiyo ambayo si ya kikazi itakayoanza Septemba 24 hadi 30.

Akiwa Tanzania, mtawala huyo wa Cambridge, atafanya mashauriano na Rais Magufuli kuhusu juhudi zinazofanywa na Tanzania katika kukabiliana na ujangili na ulanguzi wa wanyama pori, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Press Association.

Kadhalika, atazuru Bandari ya Dar es Salaam kujionea zaidi juhudi za kimaendeleo zinazopigwa na taifa hilo.

Lakini pia Lengo kuu la ziara ya mtawala huyu wa Cambridge barani Afrika ni kufuatilia juhudi za kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama.

Atafanya ziara hiyo kwa kutumia wadhifa wake kama rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama; United for Wildlife na Tusk Trust.

Amekuwa pia mlezi wa shirika la Royal African Society linalolenga kukuza uhusiano kati ya Afrika na Uingereza na hushiriki juhudi za kukabiliana na ujangili.

Inaelezwa kuwa mwaka 2009, Tanzania ilikuwa na tembo 110,000, lakini idadi hiyo imeporomoka hadi kufikia tembo 43,000 kutokana na ujangili.

William pia katika ziara yake hiyo Afrika atapigia debe mkutano mkuu wa kukabiliana na ulanguzi wa wanyamapori utakaofanyika Oktoba 11-12 mjini London.

Mkutano huo ambao kwa kirefu unafahamika kama Illegal Wildlife Trade Conference, unalenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na ulanguzi wa wanyamapori.

Utaangazia mambo makuu matatu: ulanguzi wa wanyama, wadudu na mimea, uhalifu, kujenga ushirikiano na kufunga masoko yanayotumiwa na wahalifu kulangua wanyamapori.

Taarifa ya Kensington Palace inasema ingawa atakuwa katika ziara ya binafsi, ameombwa na Malkia kutekeleza shughuli kadha rasmi kwa niaba yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles