27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Prince Harry, Meghan ‘watengwa rasmi’

LONDON, UINGEREZA

Mwanamfalme Harry na mke wake Meghan hawatatumia tena vyeo vyao vya uanaufalme na kupokea ufadhili wowote wa umma kwa ajili ya shughuli za kifalme, imetangazwa katika kasri ya Buckingham.

Wanandoa hao hawatamwakilisha tena Malkia.

Mwanamfalme Harry na mkewe wanatarajiwa pia kulipa fidia ya paundi milioni 2.4 ya pesa ambayo wananchi walitoa kwa ajili ya kujenga makazi yao, ambayo itasalia bado kuwa nyumba ya familia ya kifalme.

Utaratibu mpya utaanza mara moja baada ya msimu wa baridi mwaka huu, kasri ilieleza.

Maelezo hayo yalitolewa jana, baada ya Malkia kufanya mazungumzo na wapenzi hao siku ya Jumatatu kuhusu mustakabali wao juu ya maisha yao ya baadae, baada ya kutangaza kuwa wanataka kuacha shughuli za kifalme na kugawa muda ambao watakaa Uingereza na Canada.

Usalama wa Harry na Meghan kujadiliwa

Malkia alisema haya katika “majadiliano ya muda mrefu pamoja na haya ya sasa, nadhani kuwa kwa pamoja tumeweza kupata majibu sahihi yatakayoweza kutuongoza vyema na kuweza kurithisha wajukuu zangu pamoja na familia zao”.

“Harry, Meghan pamoja na Archie wataendelea kupendwa sana kama wanafamillia yangu,” taarifa hiyo ya malkia iliendelea.

Vilevile aliwashukuru kwa kujitoa kwa hali na mali kufanya kazi, aliongeza kusema pia haswa namna Meghan alivyoweza kuingia haraka na kuwa mmoja wa wanafamilia.

Katika taarifa nyingine, Kasri ya Buckingham ilisema kuwa:”Mwanamfalme na mke wake hawatatumia tena vyeo vyao vya kifalme na sio wafanyakazi tena wa familia ya kifalme .”

‘HRH’, ni kifupi cha ‘His/Her Royal Highness'(Mheshimiwa mwanamfalme), ikiwa sehemu ya kitamblisho kwa baadhi ya wanafamilia wa kifalme.

Mwandishi wa BBC masuala ya familia ya kifalme, Daniela Relph alisema: “Wakati taarifa ya kwanza iliposomwa kuhusu nini ambacho walikuwa wanakitaka, walizungumzia majukumu ya mwanamfalme kuwa yameondolewa yote kabisa, na haitamaanisha kuwa anaweza kutumikia nusu ya muda wake kutumikia familia ya kifalme.”

Iliongeza kusema kuwa swali litabaki kuwa halina jibu mpaka mwakani, pale ambapo wataona maisha yao ya kibiashara yataonekana yanaendaje.

“Hili ni kama jaribio au mtihani ambao wamepewa Harry na Meghan,” alisema.

Kasri ya Buckingham ilieleza kuwa wanawafalme wameelewa kuwa wanapaswa kujitoa katika majukumu ya kifalme pamoja na shughuli kijeshi.

“Hawatakuwa wawakilishi wa malkia tena, Mwanamfalme Harry ameweka wazi kuwa kila kitu ambacho watakifanya kitakuwa ni kwa mujibu wao,” ilisema.

Taarifa hiyo iliongeza kusema kuwa wanandoa hao wataendelea kuweka siri kwa kile ambacho watakuwa wanajihusisha.

Mkurugenzi wa Map Ives, na muasisi wa hifadhi ya vifaru nchini Botswana, alisema kuwa tayari alikuwa ameharifiwa na maofisa kuwa ofisi ya Harry ilikuwa inataka kuendelea na majukumu ya kifalme, kama taasisi.

“Kama kitu chochote kikitokea uhusiano wetu unapaswa kuwa imara,”  Ives alisema.

Kumekuwa na maswali mengi kuhusu nani atatoa ulinzi kwa wanawafalme hao na gharama yake itakuwaje, lakini kasri ya kifalme hawakuzungumzia lolote kuhusu suala hilo.

Harry na Meghan wana tovuti mpya inayoitwa, sussexroyal.com, iliandika pia taarifa kuhusu majukumu mapya ya Harry na Meghan.

Taarifa hiyo katika mtandao wao ilifanya tovuti yao kufuatiliwa na watu wengi kwa muda kuona jinsi walivyoondolewa kuwa waheshimiwa wanawafalme.

Mapema mwezi huu, Harry na Meghan walisema kuwa wanataka kujitegemea kifedha na kugawa muda wao ambao watatumia Uingereza na Amerika ya Kaskazini.

Mwaka jana, wapenzi hao walizungumzia wakati mgumu wanaoupata katika maisha ya kifalme kwa kila kitu wanachofanya kufuatiliwa na vyombo vya habari.

Mwanamfalme alisema kuwa anahofia mke wake anaweza kukutana na hali ambayo marehemu mama yake ilimkuta.

Malkia aliandika kuwa “siku zote wataendelea wanawafalme wapendwa katika familia ya kifalme”.

Lakini hawatakuwa na wadhifa wa kifalme wala kushughulika na shughuli za kifalme , kijeshi, kuhusika katika ziara na fedha watakazotumia Canada hazitahusisha fedha ya wananchi.

Mazungumzo ya awali yalikuwa ni namna watakavyoweza kuchanganya maisha ya uraiani na kifalme, yaani Harry na Meghan wanaweza kuendelea kufanya baadhi ya shughuli za kifalme yaani nusu kwa nusu. Lakini hali ikabadilika na kuwa ndivyo sivyo.

Lakini maisha mapya yaliyo mbele ya Harry na Meghan, umaarufu walionao, wakiwa nje ya familia ya kifalme utakuwaje.

Baadhi ya maswali kuhusu siku za mbeleni za wapenzi hao bado hayajajibiwa, ikiwa ni pamoja na suala la uhamiaji, kodi zao zitaenda Uingereza au Canada.

Haijajulikana bado kama Meghan bado ana nia ya kupata uraia wa Uingereza, na itakuwaje kama hana nia ya kukaa Uingereza muda wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles