26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

PREZZO, DOGO JANJA WAINGIA MAFICHONI

Na JESSCA NANGAWE

MSANII kutoka nchini Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’, yupo nchini kufanya video yake mpya ambayo ndani amemshirikisha msanii wa Tanzania, Abdulaziz Chande ‘Dogo Janja’.

Prezzo ameliambia MTANZANIA kuwa amekuja nchini kwa ajili ya kazi moja ya kumalizia video yake mpya ambayo anaamini itakuwa kali kutokana na jinsi Dogo Janja alivyoonyesha uwezo wake.

“Nipo Tanzania na lengo kubwa ni ‘project’ yangu na Dogo Janja, tunamalizia video ya hii ngoma kabla ya kuiachia pamoja, nashukuru ameonyesha uwezo na hajaniangusha,” alisema Prezzo.

Alisema mbali ya Dogo Janja, pia anatarajia kufanya kazi na wasanii wachanga nchini akiwemo Dogo Aslay na wengine ambao kwa sasa wanafanya vizuri kwenye kiwanda cha burudani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles