28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Pompeo yu Saudi Arabia kujadili kupotea kwa Khashoggi

RIYADHI, SAUDI ARABIA

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, amewasili mjini hapa jana kwa mazungumzo na Mfalme Mohammed bin Salman kujadili kupotea kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi.

Utata uliopo kuhusu kupotea kwa Khashoggi baada ya kuingia ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki Oktoba 2 umezitia doa juhudi za Salman za kuleta mageuzi kuboresha taswira ya Saudi Arabia duniani.

Khashoggi, raia wa Saudi Arabia anayeishi Marekani na kuliandikia gazeti la Washington Post hajulikani aliko tangu alipoingia ubalozi huo siku hiyo.

Aliingia ubalozini humo ili kupata nyaraka za kumwezesha kufunga ndoa.

Maafisa wa Uturuki wanaamini aliuawa ndani ya ofisi hiyo na mwili wake kuondolewa, madai ambayo Saudi Arabia imeyakanusha vikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles