31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI YATOA AMRI KUKAMATWA HALIMA MDEE, ESTER MATIKO

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi limetoa amri ya kukamatwa popote walipo kwa wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mbunge Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiku, kutokana na kutoripoti polisi wiki iliyopita.

Wakili wa Chadema, John Malya amesema hatua hiyo inatokana na wabunge hao kushindwa kuitikia wito uliowataka kuripoti polisi wiki iliyopita kwa sababu walikuwa wakihudhuria vikao vya kamati za bunge vinavyoendelea Mjini Dodoma.

Aidha Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika wamewekwa chini ya ulinzi kusubiri maelekezo ya kwa nini hawakuhudhuria wiki iliyopita.

“Wiki iliyopita Jumanne, wenzao waliripoti Heche na Mnyika hawakuripoti walikuwa bungeni, lakini leo wameripoti na sasa amekuja hapa Mkuu wa Upelelezi akasema mkae hapa msubiri maelekezo.

“Halima ameshindwa kuripoti, yuko nje kwa matibabu na sisi ndiyo tuko hapa tunasubiri hayo maelekezo.

Katika mwendelezo wa kuitikia wito wa kuripoti kituoni hapo, leo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji wameripoti.

Wengine waliofika kituoni hapo ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho na Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles